Home Mchanganyiko SERIKALI YA AUSTRIA NA SHIRIKA LA C.I.P WAWEZESHA MAFUNZO YA LUGHA YA...

SERIKALI YA AUSTRIA NA SHIRIKA LA C.I.P WAWEZESHA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA WAZAZI WENYE WATOTO VIZIWI-SINGIDA

0
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida, Afesso Ogenga akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya lugha ya alama yaliyowahusisha Wazazi na Walezi mkoani Singida jana.
Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika hilo Parinemas Mashanjara akizungumza katika hafla hiyo.
Afisa Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Singida, Tumaini Christopher ambaye alikuwa mgeni rasmi akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida.
Afisa Elimu Maalum wa Manispaa ya Singida Philipina Mboya akizungumzia umuhimu wa elimu hiyo.
Afisa Elimu Kata ya Misuna, Nembris August akizungumzia mafunzo hayo na kutoa shukurani kwa shirika hilo kwa msaada mkubwa wanaotoa katika shule hiyo.
 
Mkuu wa Shule ya Msingi Tumaini Viziwi, Francis Edward akizungumzia historia ya shule hiyo.
Hafla ya kufunga mafunzo hayo ikiendelea.Mshiriki wa mafunzo hayo Mnkwimba John akielezea faida aliyoipata kwa kupata mafunzo hayo.
Wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo.
Iddy Ramadhani mzazi alipata mafunzo hayo akielezea furaha aliyonao kwa kupata mafunzo hayo.
Hafla ikiendelea.
 
Wazazi wakiwa kwenye hafla hiyo.
 
Wazazi walioshiriki mafunzo hayo wakisubiri kukabidhiwa vyeti vyao.
 
Hafla ikiendelea.
 
Hafla ikiendelea.
 
Lugha ya alama ikioneshwa.
 
Lugha ya alama wakionesha wahitimu wa mafunzo hayo.
 
Hafla ikiendelea.
 
Vyeti vikikabidhiwa kwa wahitimu wa mafunzo hayo.
 
Vyeti vikitolewa.
 
Wahitimu wakionesha vyeti vyao.
 
 
 
Afisa wa Shirika la C.I.P Shabani Mukee akiwa kwenye hafla hiyo.
 
Vyoo vilivyojengwana shirika la C.I.P.
 
 
 
Muonekano wa nyuma wa Bwalo la chakula lililojengwa na Shirika la C.I.P.
Muonekano wa madarasa yaliojengwa na shirika hilo.
 
Wanafunzi wa shule hiyo wakifurahia mazingira bora ya shule yao yaliyoboreshwa kwa kiasi kikubwa na Shirika la C.I.P.
 
Wanafunzi wakifurahia mazingira bora ya shule yao.
 
 
Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 
 
************************
 
 
Na Dotto Mwaibale, Singida
 
SERIKALI ya Austria kupitia shirika la Sister Cities Salzburg –Singida (SCSS) lililoko Salzburg Austria kwa kushirikiana na shirika lisilokuwa la Kiserikali la Community Initiatives Promotion (CIP) la mkoani Singida limeendelea kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan za kuinua sekta ya elimu ambapo limewezesha kugharamia mafunzo ya lugha ya alama kwa wazazi na walezi wenye watoto wenye usikivu hafifu (viziwi) wanaosoma Shule ya Msingi Tumaini Viziwi iliyopo Manispaa ya Singida.
 
Akizungumza katika hafla ya kufunga mafunzo hayo Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la CIP , Afesso Ogenga alisema walianza kuisaidia shule hiyo tangu mwaka 2005 hadi sasa na kuwa wamekuwa wakipewa ushirikiano mkubwa na Serikali mkoani hapa.
 
Alisema tangu mwaka huo wameweza kuisaidia shule hiyo kwa kujenga madarasa mawili ofisi kuu ya zamani na vyoo vya mwanzo vya wanafunzi,jiko, Bwalo na samani zake, Magodoro ya wanafunzi 66, Matundu manne ya vyoo na chumba maalum cha wasichana na taulo zao (sodo) kwa mwaka mzima.
 
Alitaja msaada mwingine waliotoa ni sare kaptula,sketi, shati, sweta na viatu kwa wanafunzi 20 wenye mazingira magumu, vifaa vya kufundishia na kujifunzia (kamusi za Kiswahili 10, atlasi 10, kamusi ya English Kiswahili mbili, chaki na rimu.
 
Alisema pia walitoa msaada wa Photocopy machine, luninga na dishi la azam , mipira kwa michezo yote, mafunzo ya lugha ya alama ambapo mafunzo haya yaliyofikia tamati jana ni ya awamu ya tatu, ziara ya mafunzo Hifadhi ya Taifa ya Tarangire kwa wanafunzi wote na walimu na kulipia ada na stationary kwa walimu wanaojiendeleza.
 
Ogenga alisema matarajio yao kama mambo yatakwenda vizuri ni kutoa msaada mwingine kwa kutengeneza vitanda 25 (double deker), kufanya ziara ya kimasomo,kuwalipia ada walimu wawili wanaojiendeleza, msaada kwa watoto 20 wenye mazingira magumu kwa kuwanunulia sare za shule na kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
 
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Francis Edward alisema wamekuwa na mahusiano mazuri na shirika hilo tangu mwaka 2005 hadi sasa na limekuwa ni sehemu ya shule kwani wamegusa maeneo mengi katika kuifanya ionekane kama inavyoonekana.
 
.Akitoa historia fupi ya Shule hiyo alisema ilianzishwa mwaka 2001 ikiwa na jumla ya wanafunzi watano kati yao wavulana walikuwa wawili na wasichana watatu ambapo kwa sasa shule ina jumla ya wanafunzi 84, wavulana 50 na wasichana 34, walimu nane wakiume watatu na wakike watano na kuwa wanawalinzi, mpishi mmoja na mwangalizi wa wanafunzi mmoja.
 
Alisema wazazi na walezi waliotunukiwa vyeti baada ya kufuzu mafunzo hayo ni 39 na walitoka Halmashauri zote za wilaya Mkoa wa Singida, Manispaa na nje ya mkoa wa Singida.
 
Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Singida Afisa Maendeleo ya Jamii wa Manispaa hiyo, Tumaini Christopher alisema wataendelea kushirikiana na mashirika hayo kwa ajili ya kusaidi watoto wa makundi maalum na akawaomba wazazi wenye watoto wenye ulemavu wa aina yoyote wasiwafungie ndani na badala yake wawapeleke shuleni.
 
Baadhi ya miradi iliyotekelezwa na shirika hilo ni kukarabati madarasa mawili na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Ikhanoda iliyopo Halmashauri ya Wilaya Singida Vijijini na katika mwaka wa fedha 2018-2019, SCSS limetoa takribani sh. 135 milioni fedha za kitanzania kusaidia miradi ya maendeleo katika Kata za Mwasauya na Ikhanoda zilizopo katika halmashauri hiyo.