Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na timu ya mpira wa Miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye michezo ya Mei Mosi.
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana akiwa katika picha ya pamoja na timu ya mpira wa Miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye michezo ya Mei Mosi.
…………………….
Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana ameipongeza timu ya mpira wa Miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kuwa mshindi wa kwanza kwenye michezo ya Mei Mosi.
Mhe. Chana licha ya kuipongeza timu hiyo amewapongeza wachezaji na kuwataka watumie ushindi huo kama chachu ya kuongeza juhudi na ufanisi kazini utakao endana na kasi ya matokeo chanya ya Filamu ya The Royal Tour iliyozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan Jijini Arusha.
Kwa upande wake Katibu wa Michezo wa Wizara ya Maliasili na Utalii, (Maliasili Sports Club) Bi. Labi Masalu amemshukuru Mhe. Waziri Pindi Chana kwa kuiunga mkono Club hiyo ya michezo na akiahidi kutekeleza agizo alilowapa.
Michezo ya Mei Mosi hufanyika kila mwaka kwa kujumuisha wafanyakazi wote wa Serikali na Sekta binafsi ambapo kwa mwaka huu yamefanyika Jijini Dodoma na timu ya miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuibuka na ushindi.