Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Homera akifungua Kikao Kazi cha Wahariri wa Vyombo mbalimbali vya habari nchini pamoja na Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba kinachofanyika kwenye hoteli ya GR City Hoteli Mkoani Mbeya ambapo kikao kazi hicho kitajadili mikakati mbalimbali ya mamlaka hiyo katika kudhibiti dawa bandia na vifaa tiba badia pamoja na udhibiti wa matumizi ya bidhaa za Tumbaku kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo na kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyatta.
………………………………
MKUU Wa Mkoa wa Mbeya Zuberi Homera amewata wanahabari kutumia vyema kalamu na sauti zao kwa kutoa habari sahihi na zenye tija kwa jamii ili kujenga taifa imara na lenye afya.
Hayo ameyasema leo jijini Mbeya wakati wa akifungua kikao kazi kilichowakutanisha Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tina Tanzania (TMDA,) na wahariri wa vyombo vya habari kutoka Kanda za juu Kusini Homera na kueleza kuwa elimu zaidi inatakiwa kutolewa kwa jamii juu ya athari ya matumizi yasiyo sahihi dawa hali inayosababisha magonjwa sugu.
RC Homera amesema, Serikali ipo makini katika kulinda afya za wananchi kupitia Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tina (TMDA,) ambao wamekuwa makini katika kudhibiti bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na bidhaa za tumbaku kwa kuhakikisha ubora, ufanisi na matumizi sahihi ya bidhaa hiyo.
“Elimu zaidi inahitajika zaidi kwa jamii, wengi wanatumia dawa pasipo kupewa ushauri wa daktari, Niwapongeze TMDA kwa kuwa na ushirikiano na wanahabari ambao mchango wao katika kupeleka elimu kwa jamii ni kubwa…niwasihi tukatumie vyema kalamu na sauti zetu kwa kutoa taarifa zitakazolinda afya za watanzania.” Amesema.
Kuhusiana na na udhibiti wa dawa bandia mkoani humo Homera amesema, wamekuwa wakishirikiana na Mamlaka hiyo mkoani Mbeya katika kupambana na kutokomeza dawa bandia ili kulinda jamii dhidi ya madhara yatokanayo na dawa hizo.
Awali akieleza lengo la mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba ( TMDA,) Adam Fimbo amesema, katika kikao hicho watatoa elimu, kueleza majukumu yanayofanywa na Wakala hiyo, wajibu wa kila mmoja katika kulinda afya ya jamii kwa kuzuia athari zinazoweza kujitokeza kutokana na matumizi ya Dawa, vifaa tiba na vitendanishi pamoja na kujadiliana kuhusu mahitaji ya wadau ili kuboresha na kutoa huduma bora zaidi.
Pia ameeleza kuwa, elimu kwa Umma kwa Wakala hiyo ni muhimu na wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii juu uelewa na matumizi sahihi ya dawa ili kulinda afya na hiyo ni kupitia vyombo vya habari.
Fimbo amesema, licha ya Wakala hiyo kushika nafasi ya kwanza barani Afrika kwa kuwa na mifumo bora ya udhibiti wa bidhaa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi bado wanaendelea kusajili, kupima ubora bidhaa kupitia maabara zao ili mlaji apate bidhaa salama bila kudhurika.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Homera akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo wakati alipokuwa akimkaribisha kushoto ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyatta.
Kutoka Kushoto ni Kisa Mwamwitwa Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti wa Vifaa Tiba na Vitendanishi , Mkurugenzi wa Huduma za Maabara, Dkt. Danstan Hipolite na Dkt. Yona Hebron Mwalwisi Kaimu Mkurugenzi Udhibiti wa Dawa wakiwa katika kikao kazi hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw. Juma Homera akimsikiliza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyatta alipokuwa akitoa shukurani zake mara baada ya mkuu wa mkoa kufungua kikakazi hicho wa pili kulia ni
Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Gaudensia Simwanza akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya hoja zilizowasilishwa katika kikao kazi hicho.
Martha Malle Mwanasheria Mwandamizi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) akifafanua mambo mbalimbali ya kisheria na namna mamlaka hiyo inavyofanya kazi.
Chrispin Severe Mkurugenzi Uendeshaji Huduma Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba akiwasilisha mada kwa wahariri mbalimbali wa vyombo vya habari waliohudhuria katika kikao kazi hicho.
Picha mbalimbali zikionesha wahariri mbalimbali wakifuatilia mada katika kikao kazi hicho.
Baadhi ya maofis wa TMDA wakiwa katika kikaokazi hicho kulia ni Afisa mwandamizi elimu kwa umma kutoka TMDA James Ndege na kushoto ni Afisa Mwandamizi Habari na Elimu kwa Umma wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Roberta Feruzi.
Picha ya Pamoja.