Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt Damas Ndumbaro (wapili kulia) akipokea taarifa ya Kongamano la msaada wa Kisheria lililofanyika mapema mwezi wa nne jijini Dodoma. Taarifa imewasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility Bi. Lulu Ng’wanakilala, leo tarehe 25 Aprili, 2022, jijini Dodoma.
……………………………
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt Damas Ndumbaro ametaka faini zinazolipwa mahakamani ziwe chanzo cha fedha katika mfuko wa msaada wa kisheria unaotarajiwa kuanzishwa hivi karibuni.
Waziri Ndumbaro ameyasema hayo, leo tarehe 25 Aprili, 2022, jijini Dodoma wakati akipokea taarifa ya Kongamano la msaada wa Kisheria lililofanyika mapema mwezi wa nne jijini Dodoma. Taarifa imewasilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility Bi. Lulu Ng’wanakilala
Waziri Ndumbaro alisema “Moja kati ya chanzo cha fedha za mfuko wa msaada wa kisheria ni faini zinazolipwa mahakamani”
Pia Waziri Ndumbaro aliwataka watendaji wa LSF na Wizara kujifunza kuhusu uendeshwaji wa Mfuko wa msaada wa Kisheria kutoka kwa nchi nyingine kama Kenya na Zambia ambazo tayari zina mifuko hiyo.
Vilevile Waziri Ndumbaro ameshauri kuangaliwa upya kwa mfumo wa haki jinai nchini kwani unaonekana kupitwa na wakati.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Legal Service Facility Bi. Lulu Ng’wanakilala amesema wamekuwa wakishirikiana kwa karibu na Wizara ya Katiba na Sheria tangu kuanzishwa kwa sheria ya Msaada wa Kisheria mwaka 2017 katika kuwawezesha watoaji wa msaada wa kisheria ili waweze kutenda kazi zao.