Mhadhiri kutoka Idara ya Uhandisi wa Kielektoniki na Mawasiliano Ndaki ya Tehama Chuo Kikuu Cha Dar es salaam na Mratibu wa Programu ya “SmartGirlz in ICT” Khadija Mkocha akielekeza jambo wakati wa program hiyo ikiendelea.
Mwanafunzi Ilakoze Jengo kutoka Sekondari ya Alpha High School akieleza kuhusiana na App ambao wameiandaa wakiwa washiriki Katika program ya SmartGirlz in ICT ambayo imefanyika Katika Viwanja vya Ndaki ya Tehama kijitonyama Dar es salaam
Baadhi ya wanafunzi wakionyesha ujuzi wao Kwa vitendo wakati ya Program ya “SmartGirlz in ICT”
Picha ya pamoja
……………………….
NA MUSSA KHALID
Wanafunzi Nchini hususani wa kike wametakiwa kuendelea kuongeza juhudi katika kujifunza masomo ya Sayansi na Teknolojia Ili waweze kuwa na ujuzi mkubwa katika kutengeneza mifumo ya kibunifu ya Tehama.
Kauli hiyo imetolewa Leo jijini Dar es salaam na Mhadhiri kutoka Idara ya Uhandisi wa Kielektoniki na Mawasiliano Ndaki ya Tehama Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Khadija Mkocha wakati wa kufanyika Programu ya “SmartGirlz in ICT” ambayo imewahusisha wanafunzi kutoka katika Shule mbalimbali Dar es salaam.
Mkocha ambaye pia ni Mratibu wa Program hiyo amesema imeanza kufanyika Maandalizi kwa wiki tatu na kuwapata wanafunzi washindi watatu kutoka katika kila shule shiriki ambapo ni katika kuelekea kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa kike katika Tehama ambayo hufanyika kila Mwaka Alhamisi ya mwisho wa mwezi wa nne.
Dk. Mkocha amesema mifumo ya Tehama ina faida kubwa kwani inahusika katika sekta na Idara mbalimbali Duniani hivyo wanawafundisha wanafunzi ili waweze kuwa na uwezo Katika kutumia matumizi ya Tehama na kutatua matatizo katika jamii zao.
“Sasa hivi Duniani kuhusu ICT ndo kila kitu kwani hata Mtoto anaweza kuchukua simu na kuitumia Katika matumizi ya kuangali na kujifunzia masomo mbalimbali”amesema Dkt Mkocha
Aidha Dkt Mkocha amesema Programu hiyo inafanyika mwaka wa tatu Sasa ambapo wanawachukua watoto wa kike ili kuwajengea uwezo katika Tehama hivyo walioshindanishwa na waliochaguliwa katika kila shule watakwenda kushiriki na kuonyesha katika maadhimisho ya siku ya Mtoto wa kike katika Tehama nchini yatakayofanyika April 28 Mwaka huu yakiratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania- TCRA
Kwa Upande wao baadhi ya wanafunzi ambao wameshiriki Katika program hiyo ya “SmartGirls in ICT”akiwemo Mwanafunzi Ilakoze Jengo kutoka Sekondari ya Alpha High School Pamoja na Naziri Nurdin kutoka Makongo High School wamesema watahakikisha wanaendelea kujifunza masomo ya Sayansi kwa bidii Ili kuweza kuzifikia ndoto zao kupitia pia mitandao mbalimbali ambayo wanaifungua kupitia internet.
“Kweli masomo ya Hesabu huwa yanaogopwa hivyo mimi naamni kama Mwanamke akiwa na utashi wa kujifunza masomo ya ICT na Sayansi atayaona manufaa yake mbeleni”amesema Ilakoze
Naye Angelina Misso Mhadhiri Msaidizi Kutoka Chuo Kikuu Cha Dar es salaam amekuwa jaji katika program hiyo na kusema Katika washiriki zaid ya 21 wameweza kupitia walichokitengeneza na kusema wamekuwa na uwezo mkubwa katika kutengeneza vitu mbalimbali ikiwemo website,App hivyo amewataka wazazi na walezi kuendelea kuwatia moyo wanafunzi waweze kusoma wanachokipenda.