………………….
Katika kuhakikisha jamii ya watanzania inaendelea kupata habari za sayansi, Teknolojia na ubunifu WAHARIRI wa vyombo vya habari mbalimbali wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano na serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) lengo likiwa ni kuongeza tija eneo la sayansi, teknolojia na ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu na (STU) nchini.
Ahadi hiyo wameitoa jijini Dar es salaam wakati wa warsha ya mafunzo ya kutazamia nafasi ya wahariri katika uzalishaji na usambazaji wa habari za sayansi, teknolojia na ubunifu iliyofanyika hivi karibuni iliyoandaliwa na COSTECH kupitia kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa (DKM) COSTECH ili kutengeneza mkakati madhubuti utakaosaidia kuzalisha na kusambaza makala nyingi zaidi za mafanikio ya miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini ili wananchi wafahamu kazi kubwa inayofanywa kwa ajili ya maendeleo ya Taifa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Bugwesa Katale akifungua mafunzo hayo alisema COSTECH ni Taasisi ya Umma na moja ya jukumu lake kubwa ni kuishauri Serikali pamoja na kuratibu na kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu hapa nchini, kwa kuandaa agenda za utafiti za Utafiti na unadaaji wa nyaraka mbalimbali za namna ya kuongoza tafiti na bunifu zinaweza kuendeshwa hapa nchini.
“Leo tuko hapa katika kuhakikisha tunaendeleza jukumu la kusambaza habari za sayansi, teknolojia na ubunifu na ubinifu. Vilevile Tume ina Kurugenzi nne ambazo ni Usimamizi na Kurugenzi ya Uendelezaji wa Tafiti, Kurugenzi ya Menejimenti ya Maarifa, Kurugenzi ya Huduma za Taasisi na Kurugenzi ya Uhawalishaji wa Teknolojia na zinafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunapata matokeo” alisema.
Dkt. Bugwesa aliongeza pia Tume ina vitengo vinavyosaidia utekelezaji wa kazi zake na mojawapo ni Mfuko wa Taifa wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE) kazi yake kubwa ni kufadhili miradi ya utafiti na ubunifu nchini.
Kaimu Mhariri wa Gazeti la Habarileo Mgaya Kingoba, ameipongeza Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuandaa mafunzo hayo kwa wahariri kwani yamewajengea uwezo mkubwa kuelewa na kuongeza kuwa COSTECH ni wadau muhimu na wanamchango mkubwa kuhakikisha habari zinatoka kwa urahisi, COSTECH waendelee kuwashirikisha waaandishi wa habari na wahariri ili waweze kutoa taarifa katika lugha rahisi wananchi waweze kuelewa dhana nzima ya matumizi ya tafiti.
Kwa upande wake, Shinuna Said, Mhariri wa Habari kutoka TBC kitengo cha Habari na Matukio aliwapongeza COSTECH na kuongeza kuwa mafunzo haya yana manufaa zaidi ambapo yataenda kutoa habari kwa lugha rahisi na kutatua changamoto ya bunifu na matokeo ya tafiti kubaki kwenye makabati bila kuwafikia walaji wa mwisho ambao ni wananchi.
“Haya mafunzo ni muhimu kwa sisi wahariri tunaozalisha vipindi na habari mbalimbali ili bunifu na tafiti ziweze kuwafikia walengwa ambao ni wananchi” alisema.
Kabla ya kufunga mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Menejimenti ya Maarifa COSTECH, Dkt. Philibert Luhunga aliwashukuru wahariri kwa kushiriki kikamilifu
katika mafunzo hayo na kusisitiza kuja na mkakati shirikishi utakaosaidia kuendeleza ushirikiano baina yao ili kufikia matamanio ya kuendesha Taifa kwa sayansi na teknolojia na hatimae kufikia maendeleo kwa ufanisi mkubwa ili jamii ya Kitanzania inufaike kwa tafiti pamoja na bunifu.