Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Lyambene Mutahabwa akizunguza wakati wa mafunzo kwa wadau mbalimbali wakiwemo maafisa elimu wa mikoa, msingi, Sekondari pamoja na wadhibiti wakuu ubora wa shule wa Kanda na wilaya yaliyofanyika kwenye hoteli ya White Sands Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Bi Suzan Nusu Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Msingi Ofisi ya Rais TAMISEMI akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye hoteli ya White Sands Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Picha mbalimbali zikionesha baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo.
Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Lyambene Mutahabwa kulia akiwa na Meza kuu na maadhi ya wadau.
Picha ya Pamoja.
……………………………………..
Kamishna wa Elimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Lyambene Mutahabwa amesema serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imetoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wakiwemo maafisa elimu wa mikoa, msingi, Sekondari pamoja na wadhibiti wakuu ubora wa shule wa Kanda na wilaya, mbali na mambo mengine alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa wadau hao.
Kamishna Kamuhabwa amesema hayo wakati wa mafunzo ya sekta ya elimu,juu ya utekelezaji wa awamu ya pili ya Programu ya ‘Lipa kulingana na matokeo katika sekta ya elimu’ ambayo lengo lake ni kuwawezesha kuwa wabunifu na kuweka mikakati ya kutekeleza mipango kazi yao.
Programu hiyo inayoratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) lengo lake kuu ni kuwajengea uwezo watendaji hao waliopo katika sekta ya elimu nchini.
Amesema kwa kuzingatia sekta ya elimu nchini, awamu ya pili ya program ya Lipa kulingana na matokeo katika sekta ya elimu inakuja mara baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza, utasaidia kuhakikisha kuwa vipaumbele zaidi vya sekta ya elimu vinatekelezwa kwa kuzingatia mipango na bajeti iliyoidhinishwa na Bunge kwa mwaka husika.
“Mafunzo haya yamekuja wakati muafaka kwani yatatoa fursa kwa wadau wa elimu hususani wasimamizi na watendaji wa elimu katika ngazi ya kanda, mikoa na Halmashauri kufahamu kwa kina kuhusu programu hiyo” amesema Mutahabwa
Ameongeza kuwa programu hiyo iliyojikita katika maeneo sita utekelezaji wake utaiwezesha Serikali kupata fedha kupitia hiyo na hivyo kuifanya iweze kufikia malengo yake ya kutoa elimu bora kwa watoto wa kitanzania.
Amesisitiza pia kupitia mpango huo, utawawezesha washiriki hao kujadili vigezo vya kupata fedha ili kuwa na uelewa wa pamoja sambamba na kuweka mikakati thabiti ya kusaidia mamlaka za Serikali za mitaa kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa vigezo na hatimaye kupata fedha zitakazosaidia utekelezaji wa vipaumbele vya elimu.
Aidha alisema utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mpango huo umesaidia kuleta mafanikio makubwa ikiwemo kujenga utamaduni wa kutumia rasilimali zilizopo kwa ufanisi katika kutekeleza malengo ili kuleta maendeleo endelevu.
Alisema fedha zitakazopatikana kutokana na programu hiyo zitatumika katika kutekeleza vipaumbele katika elimu pamoja na kuchochea utekelezaji wake ili kuwezesha upatikanaji wa fedha zaidi.