Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameongoza mkutano maalum wa chama hicho jijini Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akiteta jambo na Katibu Mkuu wa chama hicho, Daniel Chongolo katika mkutano huo. Viongozi wakiwa meza kuu.
|
Katibu Mwenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka akizungumza kwenye mkutano huo. |
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo akihutubia kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha TLP Agustino Mrema na mke wake mpya Doreen Kimbi wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu Mstaafu wa CCM Yusuph Makamba akizungumza kwenye mkutano huo.
Kikundi cha Sanaa cha TOT kikitoa burudani kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa mkutano huo wakiserebuka.
Mjumbe wa Mkutano huo kutoka Mkoa wa Mbeya Charles Mwakipesile (wa pili kutoka kushoto) akiwa kwenye mkutano huo.
Nifuraha tupu katika mkutano huo. Kutoka kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu, Patrobas Katambi Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye.
Waziri wa Kilimo Hussein Bashe akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ya CCM (NEC) Taifa Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas. Mkutano ukiendelea.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa Mkutano huo kutoka mkoa wa Ruvuma wakati Mkutano ukiendelea.
Kikundi cha Sanaa cha All Star kikitoa burudani kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Furaha tupu kwenye mkutano huo Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi na Makazi Ridhiwani Kikwete akiwa katika Picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Ndugu Zelothe Steven.
Na Dotto Mwaibale,FULLSHANGWE
Dodoma
…………………………………..
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia
Suluhu Hassan ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ameongoza mkutano maalum wa chama hicho jijini Dodoma leo.
Akifungua mkutano huo uliohudhuriwa na wajumbe kutoka mikoa yote Rais Samia alisema utakuwa na ajenda kuu mbili kubwa ambazo ni zaimu si kwa chama hicho pekee bali na kwa taifa kwa
ujumla.
Ajenda hizo ni marekebisho kadhaa ya vipengere katika katiba ya chama hicho na uchaguzi wa Makamu wa CCM Tanzania Bara ambao unafanyika baada ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Mzee Philip Mangula kuamua kung’atuka kwa hiyari baada ya
kukitumikia chama hicho kwa muda mrefu na chama hicho kumpendekeza aliyekuwa Katibu Mkuu Mstaafu wa chama hicho Abdulrahman Omari Kinana kugombea nafasi hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo alisema mkutano huo umekidhi vigezo kwa kuhudhuriwa na idadi ya wajumbe inayotakiwa hivyo kuwa ni halali kufanyika kwa mujibu wa sheria na katiba inavyoelekeza.
Katika Mkutano huo baadhi ya viongozi mbalimbali wa chama
na Serikali wamehudhuria akiwepo Mwenyekiti wa chama hicho mstaafu, Jakaya Mrisho Kikwete, makatibu wakuu wastaafu wa
chama hicho, Rais mstaafu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein, Rais wa Zanzibar Dk.Hussein Ali Mwinyi na wanasiasa maarufu kutoka vyama mbalimbali pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha TLP Agustino Mrema ambaye aliambatana na mke wake mpya Doreen Kimbi na baada ya Rais kumtambulisha ukumbi
mzima ulilipuka kwa shangwe na nderemo.