Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumz katika mkutano Mkuu Maalum wa CCM uliomchagua wakati akiwashukuru wajumbe wa mkutano huo kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Convetion Center jijini Dodoma leo.
akamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteta jambo na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo mara baada ya wajumbe wa Mkutano Mkuu kumchagua kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara.
………………………………………
Na Dotto Mwaibale,FULLSHANGWE, Dodoma
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamempitisha kwa asilimia 100 kwa kumpigia kura 1875 za ndio Abbrahaamni Kininan kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho katika mkutano mkuu maalumu uliofanyika leo jijini Dodoma.
Akizungumza wakati akitoa shukurani kwa kuchaguliwa Kinana alisema suala la ukabila, ukanda,udini na kimkoa lisipewe nafasi katika nchi yetu na halikubaliki.
“Tutofautiana kwa hoja na si ukabila, udini, kikanda na kimkoa kwani kufanya hivyo hakutatuletea maendelea watanzania ambao tunasifika hadi nje ya nchi kwa umoja wetu” alisemaKinana.
Kinana alisema jambo la muhimu la kuzingatia kwa Wana CCM ni kuzingatia haki pale Wananchi wanapo mchagua mtu wanayemtaka aachwe na kuwa wapaswa kuilinda haki hiyo kuanzia ndani na nje ya chama.
Aidha Kinana alisema ni vizuri chama kitende haki ya kila mtu kusikilizwa kwani hakuna mtu mwenye haki miliki ya mawazo ya mtu ambapo pia alihimiza kuzingatia demokrasia katika maeneo yote.
Alisema CCM ni chama kikubwa ambacho kinakubalika hivyo ni lazima kuheshimu demokrasia na kiendelee kuwa masikio ya wananchi ambapo wakisikilizwa na kutekelezewa hayo wanayoyahitaji wataendelea kukichagua.
Alisema CCM haipokei maagizo kutoka Serikali bali kinatoa maelekezo kwa Serikali ili kusimamia sera, ilani na maelekezo kutoka kwenye chama hicho.
Kinana alisema Serikali inapokosea haitakiwi kugombezwa hadharani bali vitumike vikao vya ndani ili kupata ufumbuzi wa kupata suluhu.
Kinana alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu huo maalum kwa kumchagua na kueleza atafanya kazi kadri ya uwezo wakekwa nafasi hiyo aliyopewa bila ya kuwangusha .
“Mmenitwisha mzigo mkubwa nitaitatumikia CCM na Watanzania kwa nguvu zangu zote” alisema Kinana.
Kinana alimpongeza mtangulizi wake Philip Mangula kwa kustaafu kwa heshima na kuwa amekitumikia chama hicho kwa kufanya kazi iliyotukuka na kuwa mambo mengi mazuri alijifunza kutoka kwake.
Akizungumza baada ya kupewa nafasi ya kushukuru Mangula alisema kung’atuka katika uongozi hakumaanishi ataacha kufanya kazi za chama bali ataendelea kuwa mshauri wakati wote pale atakapo hitajika kufanya hivyo.