…………………….
Na Mwamvua Mwinyi-
Dkt. Joseph Chacha Sunguro wa hospitali ya CCBRT akimpima macho mmoja wa wakazi wa Kunduchi, Dar es Salaam katika zoezi la uchunguzi wa afya ya macho na magonjwa ya mifupa lilioendeshwa kwa pamoja katika ya hospitali ya CCBRT na kituo cha afya cha Jeshi la Polisi Kunduchi.
Zaidi ya wakazi 100 wa Kunduchi wamepatiwa huduma hiyo. Tangu mwaka 2020 taasisi hizi mbili zimekuwa zikishirikiana ili kuwa na nguvu ya pamoja katika kutoa huduma za afya kwa watanzania wenye mahitaji. Kazi ya Jeshi la Polisi ni zaidi ya kuwalinda raia na mali zao inakwenda mbali kuwalinda kiafya.