Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bw Achiles Bufure, akizungumza na Walimu, Wazazi na Wanafunzi wa Kisutu Sekindari waliotembelea Makumbusho hiyo.
Mwl Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisutu Mwl Chiku Mhado akizungumza na Wazazi na wanafunzi wa Shule hiyo, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar Es Salaam
Afisa Elimu Mwandamizi wa Makumbusho ya Taifa Bi Anamary Bagenyi akiwapatia maelezo wanafaunzi wa Shule ya Sekondari Kisutu juu ya Magari yaliyotumiwa na Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisutu wakijifunza historia ya Tanzania kwenye moja ya Maonesho yaliyopo Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Wazazi na wafanzu wa Shule ya Sekondari Kisutu wakiwa kwenye viwanja vya Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam
……………………….
Na Catherine Ngowi
Walimu, wanafunzi na Wazazi nchini wameshauriwa kutenga muda wao na kutembelea Makumbusho za Taifa ili waweze kujipatia maarifa zaidi ya uridhi wa Utamaduni na Maliasili
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam Bw Achilesi Bufure kwa Wazazi, Walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kisutu waliotembelea Makumbusho hiyo kwa lengo la Kujifunza na kuburudika kupitia programu ya Twenzetu Makumbusho.
Bw Bufure licha ya kuupongeza Uongozi wa Shule ya Sekondari Kisutu kwa kuitembelea Makumbusho hiyo, anatoa wito kwa wanafunzi hasa wa kitato cha Sita kabla ya mitihani yao kwenda Makumbusho kujikumbushia kwa vitendo yale waliofundishwa.
“Natoa wito kwa wanafunzi kujiwekea utamaduni wa kutembelea makumbusho ili kujiongezea maarifa kwa vitendo katika masomo na kuelewa historia na asili ya nchi kwa uzalendo wa nchi yao” Bw Bufure alisema
Licha ya kuipongeza Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, kuanzisha program inayowapa wanafunzi nafasi ya kujifunza kwa matendo, Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisutu Mwl Chiku Mhando amesema wanamatarajio makubwa katika ufaulu wa wanafunzi wao baada ya kujifunza kupitia Makumbusho hiyo.
“Licha ya kuja kufanyia maafali yetu hapa ya Kidato cha Sita, tumeona tutumie fursa hii kuona namna wanafunzi wetu wanavyo weza kufaidika na Makumbusho hii, pamoja na wazazi wao ambao naamini wengi wao hawakufika katika taasisi hii muhimu katika kujifunza mambo ya Historia ya nchi na uzalendo” Mwl Mhando.
Mmoja wa Wazazi waliojumuika na wanafunzi hao ameeleza kuwa amefurahishwa na utaratibu wa Shule hiyo ya Kisutu kwa kutumia njia nyingine ya vitendo zaidi kufundisha wanafunzi kwa kuwa njia hiyo licha tu ya kuwafanya waelewe haraka bali inawajenga wanafunzi kuivaa nchi yao na wao kuwa watanzania halisi.
“Mimi kama mzazi nafarijika sana kuona watoto wetu wanajifunza kwa vitendo mambo mbalimbali yanayohusu historia ya nchi yao, hivyo naipongeza Makumbusho na uongozi wa shule kwa kuandaa programu hii muhimu” aliongeza Bw Ally.
Nao Wanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Kisutu Saumu Juma na Pili Mtobi Waliopata nafasi ya kujifunza kwa vitendo na kufundisha wengine kupitia maonesho ya Makumbusho, wamesema sasa watafanya mitihani yao bila hofu na uhakika wa kufaulu ni mkubwa.
“Tunasoma vitu vingi darasani kwa nadharia, hivyo kutembelea makumbusho ni njia ya kukamilisha kwa vitendo yale tuliyoyasoma. Hii programu iwe endelevu kwa kuwa tunapojifunza kwa vitendo na kuona kwa macho ambapo ni rahisi kukumbuka hata katika mitihani yetu.” Ameeleza Saumu.
Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, imeamua kutoa nafasi kwa wanafunzi wa sekondari na Msingi kujifunza kwa vitendo masomo wanayofundishwa mashuleni na kisha wanafunzi hao kufundisha wengine na kuongoza wageni ndani ya Makumbusho hiyo.