Mkuu wa Kitengo cha Historia Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt Hezron Kangalawe akifungua warsha siku tatu ya kuwafundisha wadau namna ya kuhifadhi data ambazo zinahusiana na uhifadhi wa malikale mbalimbali ambayo inafanyika kuazia leo kwnye ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es salaam.
Mratibu wa mradi unaofanya utafiti juu ya mikusanyo iliyopo kwenye makumbusho na nyumba ya sanaa ya Dar es salaam na makumbusho ya Etholojia iliyopo Berling Ugerumani Dr Oswald Masebo akiwaeleza washiriki dhamira ya warsha hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Mawazo Ramadhani Jamvi akiwaeleza washiriki dhamira ya Makumbusho kushiriki katika warsha hiyo.
Mkurugenzi mstaafu wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Paul Msemwa (kulia mwenye shati jeupe)akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Archiles Bufure (kushoto)
Mkurugenzi mstaafu wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Paul Msemwa
Baadhi ya washiriki katika warsha siku tatu ya kuwafundisha wadau namna ya kuhifadhi data ambazo zinahusiana na uhifadhi wa malikale mbalimbali ambayo inafanyika kuazia leo kwnye ukumbi wa Makumbusho jijini Dar es salaam.
Picha ya pamoja.
………………….
NA MUSSA KHALID
Wadau wa Malikale nchini wametakiwa kuwa tayari kujifunza masuala ya utunzaji wa malikale ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa ya vitu mbalimbali kwa kuonyesha usahihi ili jamii iweze kutambua historia nya nchi yao kwa vizazi vya sasa na baadae.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha Historia Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dkt Hezron Kangalawe wakati akifungua warsha siku tatu ya kuwafundisha wadau namna ya kuhifadhi data ambazo zinahusiana na uhifadhi wa malikale mbalimbali ambazo zilikuwa zimechukuliwa na wakoloni na nyingine zipo lakini watu hawana uelewa wa namna ya kuhifadhi.
Dkt Kangalawe amesema kuwa warsha hiyo itawasaidia wadau mbalimbali wa uhifadhi kujua namna ya kuandika na kuhifadhi vifaa vya utamaduni kwa kizazi cha sasa na kijacho.
‘Sauala la uhifadhi kwa sasa kuna wadau wanaweza kuhifadhi lakini lakini bado wapo hawajaweza kuweka kwenye mfumo mzuri wa Kompyuta hivyo kupitia warsha hiyo watatambua namna ya kuhifadhi kwa haraka na kutoa tafsiri iliyo sahihi’amesema
Kwa upande wake Mratibu wa mradi unaofanya utafiti juu ya mikusanyo iliyopo kwenye makumbusho na nyumba ya sanaa ya Dar es salaam na makumbusho ya Etholojia iliyopo Berling Ugerumani Dr Oswald Masebo ametaja faida ya mradi huo kuwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi.
Dkt Masebo ambaye pia ni Muhadhiri Mwandamizi wa Historia wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam amesema pia warsha hiyo itasaidia taasisi za Makumbusho ya Taifa au Makumbusho na Malikal Zanzibar kuboresha mifumo yake ya taarifa ya mikusanyo na hivyo kuongeza ufanisi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Mawazo Ramadhani Jamvi warsha hiyo ni muhimu katika utekelezaji wa mambo yote ya kimakumbusho vikiwemo vifaa.
‘Makumbusho sasa hivi tupo katika kipindi cha mpito kubadilika kutoka katika kuhifadhi njia ya kawaida ya karatasi na kalamu na kwenda katika mfumo wa kuhifadhi wa kisasa wa kidigitali sasa sisi tunaona kama njia hii ni muhimu sana kwa kutengeneza backup’amesema Mawazo
Mshiriki kutoka Makumbusho ya Zanzibar Ibrahim Sharifu akisema mafunzo hayo yatawasaidia kupata uelewa wa kuhifadhi masuala mbalimbali kwa njia ya kidigitali.
Hata hivyo imeelezwa kupita warsha hiyo itasaidia wadau hao kuwa na ufahamu wa namna ya kuhifadhi tafiti mbalimbali za malikale na hivyo kuzifahamu changamoto zilizopo katika urithi wa taifa la Tanzania.