Katibu Tawala wa Mkoa huo, Hassan Abbas Rugwa akifungua semina ya wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) jiji la Dar Es Salaam leo iliyofanyika kwenye ofisi za Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) Posta jijini Dar Es Salaam leo.
…………………………….
Serikali imesema inatambua mchango wa wafanyabiashara maarufu Machinga katika kuchangia pato la Taifa ,hivyo imewataka kufuata utaratibu wa kuuza bidhaa zenye nembo zinazotambulika na mamlaka husika ili kuzua mianya ya uuzwaji wa bidhaa bandia ambazo nyingi zinaathari kwa mtumiaji.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala Mkoa wa Dar es salaam Bw. Hassan Lugwa wakati akizungumza na viongozi wa shirikisho la umoja wa machinga Tanzania katika semina iliyoandaliwa na tume ya ushindani Tanzania FCC.
Bw. Hassan Rugwa amesema serikali inahimiza uchumi wa viwanda kwa maendeleo ya nchini lakini suala la uzalishwaji wa bidhaa bora na zinazokubalika katika soko la ushindani ni muhimu katika ukuaji wa uchumi.
Ameongezakuwa hapo mwanzo kulikuwa na tatizo kubwa la wafanyabiashara ndogondogo kutotambuliwa mpaka Serikali ya awamu ya Tano ilipoamua kuwarasimisha rasmi ambapo sasa pia serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imesema uchumi unapokuwa ni muhimu na wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) nao biashara zao zikuwe pamoja na uchumu huo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Martha Kisyombe amesema Tanzania inapakana na Takribani nchi nane hivyo kuna kuwepo na mianya ya uingizwaji wa bidhaa bandia kwa baadhi ya wafanyabiashara wenye lengo la kukwepa kodi na kufifisha nia ya dhati ya wawekezaji wenye nia kuwekeza hapa nchini.
Amewataka wafanyabiashara hao kufuatilia kwa makini mafunzo yatakayotolewa katika semina hiyo ili yakawasaidie katika kubuni bidhaa zao na hatimaye kukuza biashara zao na kuwa tayari katika ushindani wa kibiashara kwa kuepuka bidhaa bandia.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dares Salaam ,Bw. Hassan Abbas Rugwa akifungua semina ya wafanyabiashara ndogondogo (Wamachinga) jiji la Dar Es Salaam leo iliyofanyika kwenye ofisi za FCC Posta jijini Dar Es Salaam leo kushoto ni Martha Kisyombe Kaimu Mkurugenzi Tume ya Ushindani Tanzania (FCC)
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dares Salaam ,Bw. Hassan Abbas Rugwa akimsikiliza Martha Kisyombe kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC) wakati alipokuwa akitoa maelezo kuhusu shughuli za Tume hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha wafanyabiashara hao wakiwa katika semina iliyoandaliwa na Tume ya Ushindani Tanzania FCC na kufanyika katika ofisi zao zilizopo Posta jijini Dar es Salaam leo.