Waziri wa HabariI, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh.Nape Nnauye akikagua nguzo yenye jina la Mtaa wakati wa kufuatilia utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi leo hii Jijini Mwanza
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh.Nape Nnauye akiwa na wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu wakipatiwa maelezo mbalimbali katika eneo la Mkongo wa mawasiliano ya Taifa uliopo ofisi za TTCL Jijini Mwanza
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye ( wakwanza kulia) akiwa na wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu leo hii katika ziara ya kukagua miradi ya huduma za mawasiliano Jijini Mwanza
Mwenyeki wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu Mh. Selemani Kakoso aliyetanguli akiwaongoza wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu kwenda kukagua mnara wa mawasiliano uliojengwa katika Kata ya Nyampande Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza
…………………………………..
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Zaidi ya wakazi 6000 wa kata ya Nyampande Wilayani Sengerema wanaendelea kunufaika na huduma ya mawasiliano ya simu baada ya Serikali na wadau wa maendeleo kutumia sh.Bilion 5.4 kujenga minara 40 Mkoani Mwanza.
Hayo yamebainika leo hii Ijumatano Machi 16,2022 wakati wa ziara ya kudumu ya Bunge ya miundombinu ya kukagua miradi ya huduma za mawasiliano iliyotekelezwa na Wizara ya Habari,Mawawasiliano na Teknolojia ya Habari Mkoani Mwanza.
Ziara hiyo imehusisha Ukaguzi wa ujenzi wa mnara wa mawasiliano wa Nyapande,kufatilia utekelezaji wa oparesheni ya anwani za makazi na kukagua mitambo ya Mkongo wa mawasiliano ya Taifa.
Akizungumza mara baada ya kukagua mnara wa mawasiliano wa kata ya Nyampande,Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya miundombinu, Mh.Selemani Kakoso amesema kuwa wameridhishwa na jitihada za Serikali za kupeleka mawasiliano kwa Wananchi hali inayosaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Amesema kuwa Wizara kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imefanya jambo zuri sana la kupeleka mawasiliano kwa Wananchi hususani kwenye maeneo ambayo hayakuwa kabisa na mwasiliano na hivyo kuleta mabadiliko makubwa katika maendeleo.
Kakoso amesema kuwa minara hiyo inayojengwa ikawe chachu ya kuchochea maendeleo, na kutengeneza uchumi kwa kujenga madarasa,Zahanati ili Wananchi wazidi kunufaika.
Akizungumza kwenye ziara hiyo Waziri wa HABARI, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nnauye ameileleza kamati hiyo kuwa ujenzi wa mnara huo umetekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom.
Amesema kuwa Serikali inajitahidi sana katika kuhakikisha Wananchi wake wanapata huduma ya mawasiliano na ndio maana Serikali imeipatia fedha Kampuni hiyo ya simu ili iweze kutekeleza mradi huo ambao umekuwa msaada mkubwa kwa Wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema Senyi Ngaga ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo wanawajali Wananchi katika kuwaboreshea huduma za mawasiliano kwani katika Kata ya Nyapande Wananchi wameweza kufungua biashara mbalimbali ikiwemo huduma za fedha.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose amesema kuwa wako tayari kuendelea kushirikiana na Serikali kujenga minara ili Wananchi wazidi kupata huduma za uhakika.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Justina Mashiba amesema kuwa hadi sasa ujenzi wa minara 18 imekamili na minara 22 inaendelea kujengwa ambapo inategemewa kukamilika Juni mwaka huu ambapo kiasi cha sh. Bilion 5.4 zitatumika kujenga minara hiyo itakayo wasaidia Wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni kupata huduma stahiki.
Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabliel amesema kuwa utekelezaji wa oparesheni ya anwani za makazi unaendelea vizuri ambapo jumla ya nyumba 643,298 kati ya nyumba 551,554 zimewekewa namba sawa na asilimia 118.5.
Amesema kuwa wanaendelea kutoa elimu kwa wadau ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye zoezi hilo ambalo litakamilishwa Mei 2020