Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Khadija Shaban-Keisha- (kushoto) akisalimiana leo mjini Tanga na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) wakati Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipowasili Mkoani Tanga kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Mahakama.
Na Tiganya Vincent_Mahakama ya Tanzania
Wananchi wametakiwa kutumia Kituo cha Utoaji taarifa (call center) cha Mahakama ya Tanzania kutoa maoni yao pale ambao wataona hawajaridhika na huduma waliyopatiwa.
Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Tanga na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel alipokuwa akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ambayo iko katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ya Mahakama.
Alisema lengo la Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Khamis Juma kuagiza uanzishwaji kwa Kituo hicho ni kuhakikisha haki inatolewa kwa uwazi na uhakika kwa watu wote hapa nchini muda wote.
Prof. Ole Gabriel alisema kuwa huduma hiyo inapatikana katika namba ya simu ya mkononi ya 0752500400 na barua pepe ya [email protected] kwa saa 24 mwaka mzima ambapo watoa huduma watawasikiliza na kuwapa majibu sahihi kulingana na maswali yao.
Alisema kuwa Kituo hicho ni muhimu kwa wananchi kukitumia katika kuuliza maswali na kupata majibu ambayo yatawawezesha kuondoa maduku duku waliyo nayo ambayo mengine yanasababishwa kwa baadhi ya kwa kutokuwa na uelewa na kutosha kuchukua maanuzi yasiyo sahihi.
“Kuwa na miundombinu bora na watumishi ni jambo moja ni lazima tuwe jamii iliyoelimishwa kutii sheria bila shuruti na kama kuna jambo ambalo limetokea katika jamii na hakuridhika tafadhali wasilina na Kituo hicho badala ya kuchukua Sheria mkononi” alisisitiza
Mwisho
MAELEZO YA PICHA
1.Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Khadija Shaban-Keisha- (kushoto) akisalimiana leo mjini Tanga na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) wakati Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria walipowasili Mkoani Tanga kwa ajili ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Mahakama.
2. Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda ( kushoto kutoka mlango wa basi) akisalimiana na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel(kulia) leo mjini Tanga wakati alipoongozana na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Mahakama.
3.Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (katikati) leo mjini Tanga wakati alipoongozana na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Mahakama.
4. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akitoa maelezo mafupi leo Mjini Tanga ya kuwakaribisha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo ya Mahakama.
5. Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kulia) akimuongoza Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka (katikati) na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) na Wajumbe wa Kamati hiyo (walio nyuma) kwa ajili ya ziara ya ukaguzi wa mradi wa Jengo la Mahakama Kuu kanda ya Tanga la Utunzaji nyaraka.
6.Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria Mhe. Emmanuel Mwakasaka(kulia) akiwaongoza leo Wajumbe wa Kamati hiyo kusikiliza wasilisho la Mahakama ya Tanzania la Mradi wa ujenzi wa Jengo la kuhifadhia nyaraka za Mahakama Kuu kanda ya Tanga.
7.Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Geophrey Pinda (kushoto) akitoa salamu za Serikali kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria leo walipotembelea kukagua mradi wa jengo la kuhifadhia nyaraka la Mahakama Kuu kanda ya Tanga.
8.Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto) akitoa shukurani kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria leo mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Tanga la kuhifadhia nyaraka.