Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akifungua Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha Jumatatu Machi 14, 2022.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akifungua Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha Jumatatu Machi 14, 2022 kutoka kushoto ni Nuru Ndile Kamishna Msaidizi wa Deni la Taifa na Japhet Justin Kamishna wa Deni la Taifa Wizara ya Fedha na Mipango.
Japhet Justin Kamishna wa Deni la Taifa Wizara ya Fedha na Mipango akitoa mada kuhusu deni la taifa katika Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha Jumatatu Machi 14, 2022
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba akimsikiliza Benny Mwang’onda kutoka Azam Media Mwenyekiti wa Wahariri katika Warsha hiyo wakati akitoa shukurani zake kwa wizara ya Fedha na Mipango kwa kuandaa warsha hiyo kushoto ni Japhet Justin Kamishna wa Deni la Taifa Wizara ya Fedha na Mipango.
Nuru Ndile Kamishna Msaidizi wa Deni la Taifa Wizara ya Fedha akifafanua jambo katika warsha hiyo inayoendelea kwenye ukumbi wa Hazina jijini Arusha.
Picha mbalimbali zikiwaonesha baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini pamoja na waandishi wa habari waandamizi wakifuatilia mawasilisho na mijadala mbalimbali katika warsha hiyo.
Bi Scola Malinga Afisa Habari Mwandamizi Wizara ya Fedha na Mipango akifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa.
……………………………….
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, amefungua Warsha ya siku tatu ya Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo jijini Arusha Jumatatu Machi 14, 2022.
Katika Ufunguzi huo Bw. Tutuba amesema warsha hiyo ni maalumu kwakuwa itawajengea uwezo wahariri wa vyombo vya Habari ili kufahamu mambo mbalimbali kuhusu hali ya uchumi wa nchi, Deni la Taifa, Mwenendo wa uchumi kwa wananchi na kadhalika.
Bw. Tutuba amesema “Tanzania inakopa kwa sababu inao uwezo wa kulipa, Ili ukope lazima uwe na uwezo wa kulipa na mkopeshaji hawezi kumkopesha asiye na uwezo wa kulipa, hivyo niwahakikishie kuwa nchi yetu inakopa kwa sababu ni tajiri na inao uwezo wa kulipa, Naomba niwahakikishie, wakopeshaji wote wanaoikopesha Tanzania, wanayo imani kubwa ya uwezo wa nchi yetu kulipa madeni.”
Aidha Bw. Tutuba amesema kuwa Katika mwaka huu wa fedha 2021/2022 serikali ilianza utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (FYDP 3) ambao Wizara itasimamia utekelezaji wa mpango huo ili kuchochea eneo la ushindani, kuongeza uwezo wa uzalishaji viwandani, kuchochea biashara, kuchochea uchumi wa maendeleo kupitia wadau mbalimbali.
Pia Bw. Tutuba amewahikikishia wahariri hao kuwa usimamizi wa matumizi sahihi na yaliyokusudiwa ya mikopo tuliyopata ni jambo la msingi na Serikali itazingatia kwa karibu mno.
“Niwahakikishie utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo unakwenda kama ilivyopangwa.” Alisema Bw. Tutuba.
Katika Warsha hiyo Wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango watatoa mada mbalimbali zikiwemo Muundo wa Wizara, Deni la Taifa, Masuala ya Mirathi na Pensheni kwa Watumishi wanaohudumiwa na Hazina. Lakini pia Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba atatumia fursa hiyo kuzungumza na Wananchi kupitia Wahariri kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Serikali ya Mwaka 2021/22 ataeleza mchakato wa Maandalizi ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa mwaka wa Fedha wa 2022/2023.
Pia Mhe. Waziri ataeleza mafanikio yaliyopatikana katika siku 365 za uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania