Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Mwanza kuelekea maadhimisho ya siku ya haki ya mtumiaji Duniani
Wakwanza (kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio akizungumza kuelekea maadhimisho ya siku ya haki ya mtumiaji Duniani Jijini Mwanza
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio Katika akiwa na maafisa wa Tume hiyo wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika ukumbi wa NSSSF uliopo Jijini Mwanza
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC) William Erio akipitia nyaraka mbalimbali wakati akijiaandaa kuzungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Mwanza.
………………………………………
Na Hellen Mtereko, Mwanza
Tume ya ushindani Tanzania (FCC) itaadhimisha maadhimisho ya siku ya haki ya mtumiaji Duniani ambayo huadhimishwa Machi 15 kila mwaka.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumamosi Machi 3,2022 Jijini Mwanza, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya ushindani (FCC), William Erio amesema Dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya haki ya mtumiaji kila mwaka ifikapo Machi 15, na hufanyika kwa lengo la kukuza uelewa wa haki na mahitaji ya mtumiaji ili kuwezesha kulindwa kwa haki hizo, kuheshimiwa na wadau mbalimbali.
Erio amesema kuwa maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Kumlinda mlaji katika huduma za fedha za kidigitali” ambayo imetolewa na taasisi inayo angalia haki za mtumiaji Duniani Consumer International.
Akizitaja haki za mtumiaji Erio amesema kuwa ni, haki ya kupata huduma bora na bidhaa bora, haki ya kuchagua bidhaa au huduma, haki ya kupata taarifa kuhusu bidhaa inapopatikana,haki ya kuzifikia huduma, haki ya kutoa malalamiko pamoja na haki ya kupata elimu ambayo wanaendelea kuitekeleza katika Mkoa wa Mwanza.
Amesema kuwa kilele Cha maadhimisho hayo yatafanyika Machi 15 na Waziri mwenye dhamana ya Uwekezaji, Viwanda na biashara Dkt.Ashatu Kijaji atakuwa mgeni wa heshima.
Erio amesema kwa sasa sehemu kubwa ya huduma mbalimbali Duniani zinatolewa kwa njia ya kidigitali Kama vile kulipia kodi za aridhi, mikopo, huduma za bima, manunuzi ya moja kwa moja kwenye mitandao.
“Kwamujibu wa takwimu zilizotolewa na taasisi inayojihusha na uangalizi wa haki za mtumiaji Duniani Consumer International, kufikia mwaka 2024 watu takribani milioni 3.6 Duniani watakuwa wanapata huduma za kifedha kidigitali, huku kwa Sasa takwimu zinaonyesha kwamba Dunia inawatu bilioni 7.2 hali inayoonyesha nusu ya watu Duniani watakuwa wanatumia huduma za fedha kidigitali”, amesema Erio
Amesema kuwa moja kati ya shughuli zinazo fanywa na Tume ya Ushindani (FCC) ni kuhakikisha wanamlinda mtumiaji kwa kuendelea kutoa elimu ili wazidi kuzijua haki zao.
Ameongeza kuwa katika kuelekea kilele cha siku ya mtumiaji Duniani, wamefanya vipindi vya uelimishaji katika Redio,Runinga na wanaendelea kufanya mafunzo maalum kwa wanafunzi wa Chuo cha Mt.Augustino kilichopo hapa Mwanza ili watanzania waelewe umuhimu wa haki zao na kuzifuata pindi wanapokuwa waitekeleza majukumu yao.