Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Stephan Ngailo akizungumzia mafanikio ya Mamlaka hiyo katika mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan.picha na Mussa Khalid
……………………………
NA MUSSA KHALID
Imeelezwa kuwa uwekezaji kwenye tasnia ya mbolea nchini umeongezeka katika maeneo mbalimbali ikiwemo idadi ya viwanda pamoja na uzalishaji katika serikali ya awamu ya sita.
Hayo yameelezwa Leo jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt Stephan Ngailo wakati akifanya mahojiano maalum na mwandishi wa habari hizi kuhusu mafanikio ya Mamlaka hiyo katika mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan.
Dkt Ngailo ameanza kueleza majukumu ya taasisi hiyo kuwa ni pamoja na kusimamia tasnia ya mbolea kwa kudhibiti ubora wa mbolea zote zinazozalishwa,kuingizwa na kutumika hapa nchini.
Aidha Dkt Ngailo amesema kuwa ziara ambayo aliifanya Rais Samia Burundi imesaidia kuwavutia wawekezaji kujenga kiwanda cha mbolea nchini ambapo mpaka sasa kimefikia zaidi ya asilimia 52.
“Kwa mazungumzo ya mwisho wawekezaji wamesema kiwanda kinaweza kuanza uzalishaji mwishoni mwa kati ya mwezi Juni,July na Agasti mwaka huu kiwanda ni uwekezaji Mkubwa ambapo uwezo wake kitazalisha tani laki sita aina mbalimbali za mbolea kwa ujumla wake pia itazalisha visaidizi vya mbolea chokaa kilimo tani laki tatu hivyo haya ni mafanikio makubwa ni wazi kwamba kikifikiwa uzalishaji suala la uzalishaji wa mbolea nchini utakuwa ni mkubwa’amesem Dkt Ngailo
Vile vile amesema kiwanda hicho kitatumia malighafi ambazo nyingi zinapatikana hapa nchini kama samadi ambayo inapatikana kanda ya kati ya ziwa kwa wafugaji lakini pia watatumia madini ya Phospheti ambayo yanapatikana Minjingu kwa bei ambayo ni nafuu.
Kuhusu jitihada wanazozifanya kwa kushirikiana na serikali katika kuongeza uzalishaji wa ndani wa Mbolea nchini,Dkt Ngailo amesema wameendelea kukutana na wawekezaji wazalishaji kujadili namza wataweza kuongeza uzalishaji.
“Kwa mujibu wa Takwimu kuanzia mwaka 2017/2020 tuliingiza Mbolea tani Millioni moja laki tisa sitini na mbili miambili thelathini na nane yenye thamani ya Dola Milioni miasita sabini na nane miamoja themanini na moja mia nane ishirini na tatu hivyo lengo letu ikiwezekana baada ya kutegemea asilimia 90 kutoka nje na 10 kutoka ndani iwe kinyume chake asilimia 90 izalishwe hapa ndani na 10 kutoka nje”amesema Ngailo
Katika Hatua nyingine Mkurugenzi huyo amesema changamoto waliyonayo ni pamoja na bei ya mbolea kupanda lakini pia mgogoro wa URUSI na UKRAINE unaweza kuathiri upatikanaji wa Mbolea.
Hata hivyo amewataka wadau mbalimbali wanaowekeza kwenye sekta ya mbolea kuendelea kuwekeza kwenye miundombinu hiyo kwa sababau itawalipa huku akiwaomba wakulima kuzingatia kanuni bora za kilimo.