Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga Captain Christopher Shalua akizungumza wakati wa ziara hiyo |
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia kushoto akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Kipumbwi wakati wa ziara yake |
NA OSCAR ASSENGA, PANGANI
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Captain Mussa Mandia ametoa wito kwa wavuvi na wasafirishaji Kata ya Kipumbwi wilayani Pangani Mkoani Tanga kuacha kutumia vyombo vya kubebea mizigo kwa ajili ya kusafiria badala yake watumie vile vilivyoruhusiwa kisheria.
Hatua hiyo inatokana na eneo la Kipumbwi kushamiri vitendo vya abiria na mizigo kupanda kwenye vyombo vya kusafirishia mizigo kufanya safari zao kati ya Kipumbwi kuelekea Visiwa vya Unguja na Pemba na hivyo kuhatarisha usalama wa maisha yao na mali.
Captain Mandia aliyasema hayo wakati wa ziara kuitambulisha bodi ya Wakurugenzi ya Shirika hilo ambao wapo mkoani Tanga ambapo walianzia kwa kutembelea Bandari ya Tanga na maeneo
mengine lengo ni kusikia changamoto walizonazo kwenye eneo la kipumbwi na kuona namna ya kuzifanyia kazi
Alisema kwao Kama Shirika wanasimamia ulinzi na usalama wa usafiri majini hivyo Serikali itachukua njia nzuri za usafiri bila kupoteza maisha na mali zenu hivyo alihaidia kulichukua suala hilo na kuhakikisha linafanyiwa kazi.
“Sisi kama Shirika jukumu letu ni kusimamia ulinzi na usalama niwahaidi suala la chombo cha usafiri hapa Kipumbwi tunalichukua na kuona namna linafanyiwa kazi”Alisema
“Hata leo asubuhi wakati nazungumza na Mkuu wa wilaya ya Pangani nimemueleza tutakachofanya kwa mamlaka tulionayo ni kuangalia namna ya kuboresha sheria, kanuni na taratibu
tulizonazo kufikia mahali ambapo kutakuwa na vyombo vizuri kwa ajili ya kusafisha watu”Alisema Captain Mandia
Hata hivyo aliwaambie wananchi wa eneo hilo kwamba chao kimefika serikali na watalifanyia kazi ili kuona namna ya kulipatia ufumbuzi kwa lengo la kuondosha changamoto iliyopo.
Akizungumzia suala la Light House kwenye eneo hilo,Captain Mandia alisema kwamba wao Shirika wanajukumu la kudhibiti vyombo vya usafiri hivyo watawaelekeza Bandari kwamba kila
wanaporasimisha wajitahidi kuhakikisha kuweka vitu ambavyo vinahitajika ili kuwasaidia wananchi ikiwemo kuweka (Light Huose) Taa,
Alisema taa hizo ambazo zitakuwa zikiwaka zitakuwa zikiashiria eneo husika ili kuweza kuwaepusha kupotea wanapokuwa majini wakiendelea na shughuli za uvuvi.
Kuhusu chombo cha uokoaji alisema tayari wao Tasac wanakuja na utaratibu huo na inategemea na bajeti maana nchi inasehemu
kubwa sana ya maji hivyo wamelichukua na kuona namna ya kulifanyia kazi.
“Lakini kitu ambacho mngeweza kukifanya wavuvi na
wasafirishaji mizigo wapeni elimu lugha ya kuwasiliana bahati nzuri wana simu za mikononi zinatumia satelite kwa hiyo wachukue kuna frequare ambazo wanatumia namba za simu wanazotumia kwa hapa wawasiliane na Bandari ya Tanga na Pengine Pangani ni rahisi mtu kusema tupo eneo
Fulani tunahitaji msaada ili kuweza kuwasaidia kuwaokoa wanapopata majanga baharini”Alisema Captain Mandia.