Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Onesmo Olengurumwa (kushoto) akimkabidhi cheti na tuzo ya maisha ya Mtetezi wa Haki za Binadamu Dkt Hellen Kijobisimba (kulia) ambayo imefanyika jijini Dar es salaam.
Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Onesmo Olengurumwa akizungumza na waandishi wa habari kueleza mchango alioutoa Dkt Kijobisimba na masuala ya utetekezi wa haki za binadamu.
Picha ya Pamoja wafanyakazi wa THRDC pamoja nawadau mbalimbali ambao wameshiriki katika hafla hiyo ambayo imefanyika usiku wa kuamkia leo.
…………………….
NA MUSSA KHALID
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania -THRDC umemtunuku zawadi ya tuzo ya maisha Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo Cha Sheria na Haki za Binadamu -LHRC Dkt Hellen Kijobisimba kutokana na kuonyesha mchango wake kama Mwanamke kudumu kwa muda mrefu katika masuala ya utetezi wa haki za binadamu Nchini.
Hayo yamejiri jijini Dar es salaam katika hafla ya kusheherekea siku ya wanawake Duniani ambayo imefanyika usiku wa kuamkia leo ambapo mtandao huo umesema licha ya Dkt Kijobisimba kustaafu katika kituo cha LHRC Bado ameendelea kuwa katika misingi ya utetezi wa haki za binadamu.
Akizungumza katika hafla hiyo Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu -THRDC Onesmo Olengurumwa amesema tuzo hiyo inatoa ujumbe kwa watanzania kuendeleza kuzisimania na kutetea Haki za Binadamu.
“Sisi kama mtandao wa Haki za Binadamu dhamira yetu ni kuona watetezi wanafanya kazi hiyo kwa wakati wote bila kuyumba na kusimamia kazi hiyo hivyo sisi kilichotusukuma sisi kumtambua Kijobisimba ni kutokana na kwamba historia yake na awamu yake amekuwa mstaari wa mbele na mwanamke pekee ambaye ametetea haki za wanawake na binadamu kwa ujumla’amesema Olengurumwa
Kwa upande wake Mkurugenzi Mstaafu wa LHRC Dkt Hellen Kijobisimba amesema amekuwa akiamini anachokifanya kwani kazi ya utetezi ameifanya kwa muda mrefu licha ya kukumbuna na changamoto mbalimbali.
Amesema kuwa ni vyema wanawake wakatumia fursa zinapojitokeza ikiwa ni pamoja na kusaidiana katika kufanya utetezi wa haki zao kwa kuzilinda ziweze kusimama.
‘Kikubwa ni kwamba kunawatau wanakukatisha tamaa pindi unapotaka kufanya jambo fulani kwa kukupa hofu ikiwa ni pamoja na kukupa majina yanayoweza kukukatisha tamaa hivyo ni vyema tukawa wajasiri katika masuala mbalimbali ili haki zetu sisi kama wanawake zisiweze kukiukwa’amesema Kijobisimba
Naye Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Nyanda Shuli amesema kuwa wanawake ni kundi muhimu kwani ni sehemu kubwa katika jamii kuanzia ngazi ya familia na kufanya maamuzi katika maeneo ya kazi.