Mbio za Same Rhino Tourism Fun Run zilizoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Same na kufanyika wilayani humo chini ya DC Edward Mpogoro zimefanyika mwishoni mwa wiki na kushirikisha wadau na Viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya Mwanga (Abdallah Mwaipaya), Kilimanjaro, Arusha (Said Mtanda) na Korogwe (Basilla Mwanukuzi) Mgeni rasmi akiwa ni Kamishina William Mwakilema Kamishna Mkuu wa Shirika la Uhifadhi la TANAPA.
Mkuu wa Wilaya ya Same Bw. Edward Mpogoro Katikati pichani aiongozana na mgeni rasmi Kamishna William Mwakilema Kamishna Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa TANAPA kuoka kulia katika uzinduzi wa mbio za kilomita tano za Same Rhino Tourism Fun Run, kulia kwake ni Mkuu wa wilaya Korogwe Basilla Mwanukuzi.
Baadhi ya wakuu wa wilaya ya Tanga kilimanjaro na Arusha wakiwa kwenye kwenye picha ya pamoja kwenye mbuga ya mkomazi baada ya kuona vivutio mbali mbali vya wanyama waahio katika mbuga hiyo.
DC Mpogoro akiwashukuru wadau mbali mbali waliojitokeza kumuunga mkono kwenye mbio za Same Rhino Tourism Fun Run ambazo zimeandaliwa na Ofisi yake kwa lengo la katangaza utalii wa ndani katika wilayao hiy ambayo imezungukwa na vivutio tofauti ikiwemo mbuga ya wanyama ya Mkomazi na milima ya kihistoria, amewaomba wananchi kupenda kutembelea kwenye vivutio hivyo vya kipekee ambavyo vipo wilayani Same na sehemu nyingine ndani ya Tanzania.