Mkurugenzi wa Rasilimali watu (Human Resources Director) Vodacom Tanzania Plc, Vivienne Penessis akizungumza kwenye mafunzo ya Tehama kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari mbalimbali nchini yaliyoandaliwa na taasisi ya dLab wenye lengo la kumpa ujuzi mtoto wa kike kupitia Tehama na kujiajiri mara amalizapo shule.
Wanafunzi wa kike kutoka shule mbalimbali za sekondari nchini wakionesha jinsi ya kutengeneza tovuti baada ya kupata mafunzo ya tehama kupitia mpango wa Code like a girl wenye kuwezesha Wasichana kujifunza bunifu mbalimbali kupitia mafunzo ya Tehama yaliyoandaliwa na taasisi ya dLab na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania Plc