Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi akifungua mafunzo ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya siku ya figo duniani , itakayofanyika machi,10 mwaka huu kulia ni Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr Linda Ezekiel, mafunzo hayo yamefanyika kwenye ofisi za Bohari Kuu ya Dawa Keko.
Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr Linda Ezekiel akiwasilisha mada katika mafunzo ya waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya siku ya figo duniani , itakayofanyika machi,10 mwaka huu.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Bohari ya Dawa MSD Bi. Etty Kusiluka kulia akifafanua jambo mara baada ya Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr. Linda Ezekiel akiwasilisha mada katika mafunzo hayo.
Mkurugenzi Bohari ya Dawa MSD Brig. Jen. Dkt. Gabriel Saul Mhidze akitoa salamu zake kwa waandishi wa habari waliohudhuria katika mafunzo hayo.
Mdhibiti Ubora kutoka Bohari ya Dawa(MSD) Joseph Kitukulu akiwasilisha mada kuhusu mashine zinazotmika kusafisha figo za wagonjwa.
Picha mbalimbali zikiwaonesha waandishi wa habari wakiwa katika mafunzo hayo yaliyofanyika leo kwenye makao makuu ya Bohari ya Dawa MSD Keko jijini Dar es Salaam.
……………………………………………
UAGIZAJI wa mashine za kusafisha Damu kwa wagonjwa wa Figo moja kwa moja kutoka kwa watengenezaji uliofanywa na Bohari ya Dawa(MSD) unaelezwa utapunguza kwa nusu ya gharama za kupata huduma hiyo hapa nchini.
Mratibu wa Mgonjwa ya Figo, Wizara ya Afya, Dr. Linda Ezekiel amebainisha hayo kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelekea maadhimisho ya siku ya Figo, Machi,10 mwaka huu.
Amesema kuwa mara ufungaji wa mashine ukikamilika, husuma hiyo itapatikana katika hospital zote za serikali.
Dr. Ezekiel amesema kuwa Serikali kupitia Bohari ya Dawa(MSD) imeagiza tayari mashine 171 za kusafisha Damu,mashine za kuchakata maji 11,mashine za kuchakata vitenganishi vya unga 26.
” Katika kipindi cha mwaka mmoja cha awamu ya sita, serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilion moja katika huduma za usafishaji Damu.Matarajio ni kuwa baada ya ufungaji wa mashine hizo huduma itapatikana kwa gharama nafuu zaidi,”amesema.
Ameaongeza kuwa ugonjwa wa Figo ni tishio kwa sasa kwani unahitaji rasilimali nyingi ili kupata huduma za afya.
Daktari huyo bingwa alisema takwimu zinaonyesha kuwa kuna takribani wagonjwa 1000 wana matatizo ya figo nchini.
amebainisha kuwa kati ya wagonjwa 5800 and 8400 wanaohitaji huduma ya kusafisha damu, 2750 tu wanapata huduma hiyo.
Naye Mdhibiti Ubora kutoka Bohari ya Dawa(MSD) Josepgh Kitukulu amesema kuwa serikali inatumia zaidi ya billion 29,484 kwa mwaka kufanya huduma ya kusafisha damu kwa wagonjwa 1000.
Katukulu amesema kupitia Bohari ya Dawa itaokoa zaidi ya bilioni 13.338 na hivyo kuboresha upatikanaji wa huduma nyingi zinazoambatana na hizo.
“Mipango yetu ni kuona watu wanapata huduma hii ya usafishaji damu katika bei nafuu,” alisema Katukulu.
Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani hufanyika Kila mwaka siku ya alhamisi ya pili ya mwezi machi ambayo mwaka huu imeangukia tarehe 10.