Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akiwa amevaa Kofia kichwani ambayo imeshonwa na wajasiriamli waliopo katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akiangalia na kukagua baadhi ya nguo ambazo zimeshonwa na wajasiriamali waliopo katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akivishwa moja ya nguo ambayo imeshonwa na wajasiriamali waliopo katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akipita katika maeneo mbalimbali yaliyopo katika Kijiji cha Makumbusho jijini Dar es salaam.
…………………
NA MUSSA KHALID
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja amewataka wanawake nchini kutumia fursa mbalimbali katika kuwekeza kwenye sekta ya utalii ili waweze kujiendeleza kiuchumi.
Naibu Waziri Masanja amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye hafla ya Mwanamke na Utalii ambayo imefanyika katika kijiji cha Makumbusho iliyoandaliwa na wanawake wa Makumbusho ya Taifa ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 ya kila mwaka.
Naibu Waziri Masanja amesema kuwa wanawake wamekuwa wakishirika katika ujenzi wa masuala mbalimbali ikiwemo kuwekeza katika sekta ya utalii hivyo amewataka kutumia fursa zinapojitokeza ili kuweza kujipatia kipato.
‘Hakika sisi wanawake kwa sasa hivi tunanyanyuka na kwenye utalii niendelee kuwa hamasisha kuwa kuna fursa nyingi kwani mtalii anapofika eneo moja wapo lenye kivutio hawezi kuingia na kukaa bali kuna vitu vingi atakavyovifanya kama atakula,atakunywa vinywani vitu mbalimbali ambavyo tunaviandaa’amesema Naibu Waziri Masanja
Aidha ametoa ujumbe kwa wanawake kuendelea kuhamasisha utalii wa ndani na kuwekeza katika sekta ya utalii kwani anaweza kujijngea uchumi kupitia fursa mbalimbali zinazotokana na utalii.
Kwa upande wake Muhifadhi katika Kijiji cha Makumbusho,Agnes Robati amesema kijiji cha Makumbusho kimekuwa kikiwaelimisha wananchi kuhusu kutambua urithi wao ikiwa ni pamoja na kutumia vyakula vya asili,kujua mila na desturi na ngoma za asili.
‘Lnego letu ni kuhakikisha kwamba tunawarithisha watoto wtu kizazi kilichopo na kijacho waju utamaduni wa mtanzania lakini pia mwanamke na mtalii tunawasaidia wajasiriamali wanaotengeneza njia za asili ili kuweza kujipatia wageni watakao waunga mkono katika biashara zao’amesema Agnes
Naye Arietha Bernad kutokea Sumbawanga Mkoa wa Rukwa amesema katika dumuisha siku ya wanawake amekuwa akitumia juhudi kufanya shughuli za ujenzi ambazo amerithishwa na wazazi wake hivyo amewataka wanawake kutolemaa badala yake washiri katika ujenzi wa masuala mbalimbali.
Hata hivyo watanzania wamekumbushwa kujiwekea mazoea ya kutumia na kula vyakula vya asili ili kuendeleza mila na desturi kwa jamii na hivyo kufanya wageni kutambua urithi wa mtanzania na sio kupenda kutumia vitu vya nje ya nchi.