Mkurugenzi Mtendaji na Muanzilishi Mwenza wa Shirika la Vijana wenye ulemavu (YoWDO) Rajabu Mpilipili wakati akitoa mafunzo kwa wanahabari ambayo leo imefanyika kwenye ofisi zao zilizopo Mbezi Beach jijini Dar salaam.
Msimamizi Mkuu wa miradi wa Shirika la Vijana wenye ulemavu (YoWDO) Genarius Ernest wakati akizungumza kwenye warsha ya mafunzo kwa wanahabari ambayo imefanyika kwenye ofisi zao zilizopo Mbezi Beach jijini Dar salaam.
George Celestine akiongoza mjadala kwa wanahabari kwenye warsha ya mafunzo ambayo imefanyika kwenye ofisi zao zilizopo Mbezi Beach jijini Dar salaam.
Wanahabari wakisikiliza kwa makini mafunzo wanapewa na viongozi kutoka Shirika la Vijana wenye ulemavu (YoWDO) wakijengewa uelewa namna ya kuandika habari zinazohusu watu wenye ulemavu imefanyika kwenye ofisi zao zilizopo Mbezi Beach jijini Dar salaam.
Picha ya pamoja(Mussa Khalid)
………………………..
NA MUSSA KHALID
Wanahabari nchini wametakiwa kushirikiana na taasisi zinazowahudumia watu wenye ulemavu kwa kuwa mabalozi watakao ielimisha jamii ili iweze kubadilika na kuepukana na changamoto za kunyanyapaliwa kwa watu hao.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es salaam na Msimamizi Mkuu wa miradi wa Shirika la Vijana wenye ulemavu (YoWDO) Genarius Ernest wakati akizungumza kwenye warsha ya mafunzo kwa wanahabari ya kuwajengea uelewa namna ya kuandika habari zihusuzo watu wenye ulemavu.
Ernest amesema kuwa malengo yao ni kuwajengea uwezo ili waweze kutoa taarifa za watu wenye ulemavu wazipokee kwa mtazamo chanya asione kana ananyanyapaliwa au kutengwa na jamii.
‘Ni matumaini yangu kuwa kwa mafunzo haya wamekuza uelewa wa kutambua ulemavu ni nini changamoto wanazozipitia,mitazamo mbalimbali kwenye jamii kuhusiana na ulemavu hivyo kupitia muongozo huu tunategemea wataielimisha jamii vilivyo’amesema Ernest
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji na Muanzilishi Mwenza wa Shirika la YoWDO Rajabu Mpilipili amesema mafunzo hayo yatawasaidia kufahamu njia mbalimbali za kuwasiliana na watu wenye ulemavu.
Aidha amesema matarajio yao ni kuhakikisha kwamba wanakwenda kuibua masuala yahusuyo watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwa chanzo cha kuibu fursa kwa vijana na watu wenye ulemavu nchini badala ya kuandika taarifa ambazo zinahamasisha misaada inayodidimiza uwezo wao.
‘Mafunzo haya yatawasaidi kufahamu namna ya kutumia majina sahihi yanayoheshimu utu wa mtu mwenye ulemavu kuliko ambayo yalikuwa yakitumika awali ambayo hayaonyeshi utu’amesema Mkurugenzi huyo Mtendaji
Nao baadhi ya waandishi wa habari ambao wameshiriki kweny Mafunzo hayo akiwemo Mwanahabari wa Gazeti la Majira Penina Malundo pamoja na Prosper Rutaruga wamesema mafunzo yamewasaidia kufahamu hasa matumizi sahihi ya lugha wanazotumia watu wenye ulemavu.
Wamesema kuwa watahakikisha wanandelea kutoa elimu kwa kutumia makala mbalimbali zitakazowasaidia wananchi wa mijini na vijijini Kupata uelewa wa kutosha kuhusu watu wenye ulemavu.
Imeelezwa kuwa kwa mujibu wa Mkataba wa Haki za watu wenye ulmavu (UNCRPD,2006) watu wenye ulemavu ni pamoja na wale wenye udhoofu wa muda mrefu wa maumbile,akili au fahamu ambao ukichangamana na vikwazo mbalimbali vinaweza kuzuia ushiriki wao kikamilifu katika jamii.