Benki ya NMB imechezesha Droo ya mwezi wa pili wa MastaBata kivyakovyako jijini Dodoma na kuwazawadia Wateja wao jumla la Tsh Milioni 25.
Tabasamu la mwanzo wa mwezi limewadodokea Wateja 25 wa NMB ambao kila mmoja aliibuka na kitita cha Tsh Milioni 1 kutoka kwenye droo hiyo.
Mastabata kivyakovyako ni droo inayochezeshwa na Benki ya NMB kwa wateja wanaotumia kadi za Mastercard kwa kufanya malipo kupitia POS au kwa kuscan QR code na kufanya manunuzi mitandaoni.
Hadi jana zaidi ya wateja 800 walishajinyakulia kitita cha Sh 100,000 kwa kila mtu wakaingia droo ya mwezi ambayo imewafikia watu 50 kwa kiwango na kuondoka na Tsh Milioni 1 kila mmoja, huku wengine 30 wataibuka na Sh milioni 3 kila mmoja kwa droo ya mwisho.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki hiyo Nsolo Mlozi alisema jana kuwa washindi wa jana walikuwa katika droo ya mwezi ambayo kila mshindi anaondoka na kitita cha Sh Milioni 1 kwenye shindano lililoanza Desemba 24,2022.
Washindi wataendelea kuchukua zawadi zao hadi droo ya mwisho ya shindano hilo ambalo limetengewa Sh 200 milioni na zote zitawafikia wateja.
Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Ibrahim Sikana alisema mchezo huo umekuwa na manufaa kwa wateja na Serikali na kuwa bodi inafurahia uwepo wake.
Sakana alisema kwa namna ilivyo, NMB inaweza kuwa moja ya taasisi za kifedha zinazoaminika zaidi kwenye droo zake kwani hakuna malalamiko yoyote toka kwa wateja wao.
Wateja wengi waliokuwa ndani ya benki ya NMB tawi la Dodoma walikusanyanyika kushudia droo hiyo ambapo wengi walifurahi kuwa ilikuwa imichezeshwa kwa uwazi na haki.
Mteja Marius Mazengo alisema hakuwa na taarifa za namna gani huwa wanashinda lakini alivyotazama jana aliona kuwa mchezo huo ni haki.
Kwa Kuwa umri wake umekwenda, mara nyingi haji benki anatumia kadi kwa kukwepa foleni, kwa hiyo kumbe na yeye yupo kwenye orodha ya kushinda na iko siku najua nami nitashinda- Mazengo.