Mfalme Mmbelwa V wa Malawi Dkt Aupson Ndabazake Thole, akizungumza kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea Mhe Michael Mbano, akizungumza kwenye ufunguzi wa Kongamano la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni
Mmoja wa washiriki akichangia mada kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Umaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni.
Wazee mbalimbali wakifuatilia mjadala kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni
Wanafunzi mbalimbali wakifuatilia Kongamano la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni
……………………
Na Sixmund J. Begashe
Tanzania imepongezwa kwa hatua mbalimbali inazozichukuwa katika kuhifadhi urithi wa kihistoria na utamaduni kwa njia ya Matamasha, Makongamano, Makumbusho za Taifa pamoja na kushirikisha wanafunzi kwenye program elimishi ukilinganisha na nchini Malawi.
Hayo yamesemwa na Chifu Mmbelwa V wa Malawi Dkt Aupson Ndabazake Thole alipokuwa akichangia mada kwenye Kongamano la Kumbukizi ya Vita vya Majimaji na Utalii wa Umaduni ambalo ni sehemu ya kuadhimisha miaka 115 ya Mashujaa waliopigania utu wa watanzania kutoka kwa wakoloni.
”Naipongeza Serikali ya Tanzania kwa kazi nzuri inayoifanya ya kuhakikisha urithi huu wa historia unahifadhiwa na kuendelezwa vizuri hasa kupitia matamasha haya na ushirikishaji wanafunzi kwenye makongamano na shughuli zingine za kiutamaduni, sisi kama Malawi tutakwenda kufanya kama mnavyo fanya.” Mfalme Mmbelwa V
Akifungua kongamano hilo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea, Mhe Michael Mbano amesema Serikali ya Mkoa wa Songea inawahakikishia wazee wa Mila na Desturi pamoja na wananchi kuwa itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha uhifadhi wa Utamaduni wa watu wa Ruvuma unakuwa endelevu
Mhe Mbano ambae ni kitukuu cha Shujaa Songea Mbano, amesema kwa kushirikana na Makumbusho ya Taifa Tawi la Songea wameendela kuwa na program nyingi elimishi kwenye shule za Msingi na Sekondari ili kuhakikisha kizazi kilichopo kinauelewa mpana wa historia ya Mashujaa wa nchi hii.
Mhifadhi wa Makumbusho ya Majimaji, Bw Baltazari Nyamusya ameeleza sababu ya kuwakutanisha wazee wa mila, machifu, viongozi wa serikali, wanafunzi na viongozi taasisi mbalimbali kwenye mjadala wa kujadili uhifadhi wa urithi wa Utamaduni wa Mkoa wa Ruvuma kuwa ili kuwa na uwelewa wa pamoja juu ya urithi huo
”Hii ni program ndani ya maadhimisho, zipo mada kadhaa zimewasilishwa hapa zikiwemo Historia ya Vita vya Majimaji, Sayansi ya kabila la Wangoni na Maendeleo endelevu ya Tanzania pamoja na Vipera vya Utamaduni, mada zilizo amsha mjadala mzito miongoni mwa waudhuriaji” Bw Nyamusya
Bw Nyamusya amesema wao kama Makumbusho ya Taifa wanamatarajio makubwa ya matokeo chanya ya kongamano hilo kwani ushiriki wa makundi mbalimbali utaifanya jamii iendelee kudumisha utamaduni na mila za makabila ya watu wa ruvuma.
Akiwasilisha mada inayohusu ” VIPERA VYA UTAMADUNI” Mwl Hilda Kapinga ameishauri serikali kuboresa vipera vya utamaduni kama vile Nyumba, Uchongaji, Maeneo ya Kihistori, Mavazi, Vyakula vya alisi, kwa kuwa vipera hivi vimekuwa ni vivutio muhimu kwa watalii wa ndani na nje.
”Vipera hivi vikipewa kipaombele hakika tutaingiza wageni wengi sana nchi maana vinapendwa na vinabadilisha ladha ya katika sekta ya utalii, lakini pia vitakuwa ni sehemu ya utatuzi wa changamoto ya ajira nchini maana vijana wengi watakimbilia kujiajiri kupitia vipera hivyo” Alisema Mwl Kapinga
Wanafunzi wa Ibrahim Juma Omary wa shule ya Sekondari Emanuel Nchimbi na Beriana Cheo Mwanafunzi wa Shule ya Wasichana Songea licha ya kuipongeza Makumbusho ya Taifa kwa kuwashirikisha katika kongamano na wao kupata nafasi ya kutoa maono ambayo ni katika kuishauri serikali kuanzisha matamasha mengi zaidi ya kihistoria ili yasaidie katika uhifadhi wa historia