Mama wa Mila wa Mkoa wa Ruvuma, Ni Zainabu Mangoma akiwafafanulia jambo kuhusu vyakula vya asili baadhi ya washiriki wa Tamasha la Kumbukizi ya miaka 115 ya MASHUJAA wa Vita vya Majimaji na Utamaduni.
Vyakula vya asili vikiwa tayari kwa kuliwa
Mgeni kutoka Ujerumani akila chakula cha asili cha Mkoa wa Ruvuma, Kwenye Tamasha la Kumbukizi ya miaka 115 ya MASHUJAA wa Vita vya Majimaji na Utamaduni
Baadhi ya akina mama wa Mkoa wa Ruvuma wakila chakula cha asili ya Mkoa huo.
…………………………..
Na Sixmund Begashe
Wanawake Mkoa wa Ruvuma wamejitokeza na kulipamba Tamasha la kumbukizo ya Miaka 115 ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni linalofanyika Mjini Songea kwa kuandaa vyakula vya asili ya makabila ya Mkoa huo ili kuwakumbusha watanzania umuhimu wa vyakula hivyo.
Akiongea kwenye Tamasha hilo, Mama wa Mila wa Mkoa wa Ruvuma Bi Zainabu Mangoma amesema, vyakula hivyo vilitumiwa na wazee wao walio pigana vita hivyo na kuwa sehemu ya ushujaa wao ulitokana na kula vyakula vilivyo imarisha afya na nguvu ya miili yao hivyo hawanabudi kuwaaenzi.
Bi Mangoma anatoa wito kwa Watanzania wote kuudhurua Tamasha hilo hasa wakazi wa Mkoa huo ili kujikumbusha mambo muhimu ya mila na desturi ambayo ni muhimu kwa ustawi wa nchi kwa ujulma
Bw Frank Kipanga anaeshiriki katika maadhimisho hayo ameeleza kuwa moja ya kilichomvutia zaidi kwenye ni ushiriki wa akina mama hao hasa kupitia vyakula vyao vya asili vyenye ladha nzuri na tofauti na alivyo zoea kula kila siku.
“Kina mama hawa kwangu wamekuwa walimu wakubwa, vyakula vyao vimenivutia sana, nimekula na sikuhisi kuacha kula maana ni vitamu sana, na huwezi kuamini mboga zingine zimetokana na majani ambayo sisi huwa tunayaona ni dawa za vidonda na chakula cha mifugo” Bw Kipanga
Akizungumzia changamoto za kiafya kwa sasa Bi Ania Suleiman amesema walio wengi wanadhani kufuata mila na desturi ni kupotea kumbe ndiko kutojiingiza kwenye matatizo makubwa hasa ya kiafya kama vile magonjwa ya Saratani, Kisukari, Presha, upungufu wa Nguvu za Kiume kwa vijana na magonjwa mengine.
Maadhimisho hayo ya Mashujaa wa Vita vya Majimaji na Utalii wa Utamaduni hufanyika kila mwaka tarehe 22 hadi 27 Februari Mjini Songea kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi za Serikali na binafsi, wazee wa Mila na Desturi Mkoa wa Ruvuma, Machifu wa Makabila mbalimbali wa ndani na nje ya nchi