…………………………
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) unaendesha semina elekezi kwa wanachama wapya 29 wa mtandao,Semina hii inalenga kuwapitisha wanachama hao wapya kuhusu sera,kanuni na misingi inayoiongoza THRDC.
Semina hiyo ya siku mbili inayofanyika jijini Dar es salaam imeanza hii leo Februari 24 na itahitimishwa rasmi hapo kesho Februari 25,2022 .Wanachama wanaopatiwa mafunzo ni wale waliofanikiwa kuwa sehemu ya Mtandao kwa mwaka 2021.
Akizungumza wakati wa Kufungua semina hiyo, Meneja Programu wa THRDC, Remmy Lema amesema semina hiyo itawapa fursa wanachama wapya kuweza kujadli mambo mbalimbali yanayoiongoza THRDC kama Mtandao na pia namna gani wanaweza kushirikiana na taasisi za kiserikali katika kutekeleza mipango na ajenda zao.
“Katika siku hizi mbili tutaweza kukaa na kufikiria na kuona ni mikakati gani ambayo tunaweza tukaitumia sisi kama watetezi wa haki za binadamu kuweza kushirikiana na serikali na kuweza kupush ajenda zetu na kukaa nao meza moja kujadiliana kuona namna ambayo jambo linaweza kwenda kidiplomasia,”amesema Remmy Lema.
Aidha ameongeza kuwa wanachama watapata nafasi ya kutafakari na kuona namna mbalimbali wanazoweza kuzitumia ili kushirikiana na aerikali na mamlaka mamlaka zingine zilizopo katika maeneo yeo wanayofanyia kazi.
“Kama mtandao kuna taratibu ambazo tumejiwekea kama mkipitia baadhi ya nyaraka za Mtandao ambazo nyingi zimetungwa na wanachama au sekretarieti ilizifanyia kazi zikatumwa kwa wanachama na wanachama wakazibariki zikapitishwa kwenye mkutano mkuu,Kuna sera ya wanachama ambayo ipo inaelezea namna ya kujiunga uanachama, nini cha kufanya, nini sio cha kufanya kwa ujumla wake vilevile vitu vyote vimezungumziwa kwenye ile sera ya wanachama,”ameongeza Remmy
Pia ameeleza kuwa wanachama hao watapitishwa katika kanuni mbalimbali za Mtandao ambazo zinaongoza wanachama ikiwemo mwongozo kwa wanachama ambao wanataka kuwania nafasi za kisiasa.
“hatuwezi kusema sisi kma wanaAZAKI tunaoperate katika mazingira ambayo ni ya utofauti sana na wakati mwingine unataka kuingia katika mazingira ya kisiasa na vitu vingine kama hivyo kuna miongozo ambayo ipo iliyopitishwa mwaka 2019 kuwa kama mwanachama wa mtandao ukitaka kujiunga kwenye harakati za kisiasa ni utaratibu gani unatakiwa kuuchukua ili uweze kuondoka na kuingia katika siasa,”
Pia amewaeleza wanachama hao kuwa katika semina hiyo watapitihswa kuhusu miongozo mbalimbali na namna gani wanaweza kushirikiana wakiwa katika kanda zao na sheria mbalimbali za kitaifa na Kimataifa na namna ambavyo wanawea kufuata sheria wakati wakitekeleza majukumu yao.
“tutapitihswa kwenye sheria mbalimbali labda hizi NGO Act, sheria ya fedha na sheria zingine zote ambazo zitakufanya tu wewe kama mwanachama wa Mtandao uweze kutekeleza majukumu yako bila kuvunja sheria na kwa uhuru.
Kwa upande wake Mratibu wa THRDC Kanda ya Dar es salaam, Michael Marwa amewataka wanachma hao wapya kuwa ‘active’ kwenye kazi zao za utetezi wa haki za binadamu pamoja na kulipa ada ya uanachama kwa wakati ili waweze kuendelea kuwa wanachama hai wa Mtandao.
Pamoja na hayo,wanachama hawa watapitishwa katika sheria mbalimbali zinazoongoza Mashirika yasiyo ya kiserikali, kuanzia usajili wake hadi ripoti. Elimu hii ni ya msingi ili kuepuka kuadhibiwa kisheria.
Waratibu wa kanda zenye wanachama wapya wamepata kuhudhuria mafunzo haya pia. Hii ni kwa nia ya kuwapa nafasi ya kuwafahamu waratibu wao wa kanda, na pia kutengeneza mashirikiano mazuri kati ya wanachama wapya na waratibu wao.