…………………………
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amewataka askari Polisi kutumia weledi na nidhamu kwa manufaa ya Jeshi hilo na kwa manufaa ya wananchi hasa pale wanapotoa huduma kwa jamii.
IGP Sirro amesema hayo wakati wa sherehe za mahafali ya sita ya Vyuo vya Taaluma vya Polisi yaliyofanyika Kurasini Dar es slaam, ambapo amesema kuwa mafunzo yanayotolewa na vyuo ya Polisi yanalenga kuinua kiwango cha ujuzi na kuwaongezea maarifa askari Polisi katika kuboresha utendaji kazi za Jeshi hilo.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Vyuo vya Polisi Profesa Frolence Luoga amewaambia wahitimu hao kutumia elimu waliyoipata katika kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha suala la usalama wa raia na mali linazidi kuimarika.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Polisi Moshi mkoani Kilimanjaro SACP Ramadhani Mungi wakati akitoa tathimini ya uendeshaji wa vyuo ya Polisi amesema kuwa jumla ya wahitimu 305 waliohitimu leo watatumia ujuzi na maarifa waliyoyapata kwenye elimu zao kwa kutoa huduma bora na zenye viwango.