Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msima akizungamza wakati akifunga semina ya waandhishi wa habari za Uchumi,Biashara na Fedha iliyokuwa ikifanyika jijini Mbeya kuanzia Februari 14 mpaka Februari 18, 2022.
Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msima ajizungumza wakati akifunga semina ya waandhishi wa habari za Uchumi,Biashara na Fedha iliyokuwa ikifanyika jijini Mbeya kuanzia Februari 14 mpaka Februari 18, 2022, Kushoto ni Mwenyekiti wa Semina hiyo Bi Dorcas Mtenga kutoka kituo cha Luninga cha Channel Ten.
Mwenyekiti wa Semina hiyo Bi Dorcas Mtenga kutoka kituo cha Luninga cha Channel Ten akimkaribisha mgeni rasmi tayari kwa ajili ya kufunga semina hiyo iliyokuwa ikifanyika kwenye tawi la BoT mkoani Mbeya.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi wakati alipokuwa akifunga semina hiyo.
………………………………………..
Tangu kuanzishwa kwa semina hizi mwaka 2013, hadi hivi sasa, kumekuwa na maendeleo makubwa namna taarifa mbalimbali zinazotolewa na Benki Kuu zinavyotumiwa na wanahabari pamoja na vyombo vyenu vya habari, Uelewa miongoni mwenu umeongezeka sana na hata ushirikiano pia umekua.
Haya ni manufaa makubwa ya semina hizi. Benki Kuu itaendelea kuzitumia semina kama hii kama sehemu mojawapo ya kushirikiana na wadau wake muhimu.
Hayo yameelezwa na Kaimu Meneja wa Uhusiano na Itifaki Benki Kuu ya Tanzania BoT Bi. Vick Msima wakati akifunga semina ya waandhishi wa habari za Uchumi,Biashara na Fedha iliyokuwa ikifanyika jijini Mbeya kuanzia Februari 14 mpaka Februari 18, 2022.
Amesema kwa sehemu kubwa ya washiriki wa semina hii, zaidi ya asilimia 70, wanashiriki katika semina hizi kwa mara ya kwanza. Tunashukuru kwa mwitikio wenu na ushiriki wenu pia.
“Kupitia michango na maswali yenu, tumetambua kwamba elimu tunayotoa inaingia, japokuwa inatakiwa kuzidi kuwajenga ili muive zaidi katika kuandika Habari za biashara, uchumi na fedha, pamoja na zile zinazoihusu Benki Kuu,” Amesema Bi. Vick Msina
Aidha amefafanua kuwa benki kuu inaamini kwamba elimu mliyoipata na mtandao ambao mmeujenga kupitia semina hii, vitaendelea kuwa faida kwenu mnapofanya kazi zenu na kwamba kwa sasa mtakuwa mmeongeza kwa kiasi fulani uwezo wenu wa kuandika habari za uchumi, biashara na fedha, hususan zinazoihusu Benki Kuu ya Tanzania na sekta ya fedha kwa ujumla.
“Ili semina hii iwe ya manufaa kwenu washiriki, mnatakiwa mjiwekee mipango ya kujipima jinsi ambavyo mnatumia elimu hii katika kazi zenu. Pia, kwa kuwa mawasilisho yote yaliyotolewa katika semina hii mnayo, ni vizuri kuyatumia kwa kujielimisha zaidi na kama rejea ya kazi zenu,” Amesema Vick Msina.
Amesema pamoja na mambo mengine, mmeweza kujenga mtandao na maafisa wa Benki Kuu waliotoa mada, ni vema mkawatumia mara kwa mara kama mnahitaji ufafanuzi wa masuala mbalimbali. Hata hivyo, mkumbuke kwamba msemaji wa Benki Kuu ni Gavana, hivyo mkitaka ufafanuzi kutoka kwa maafisa wetu, siyo tiketi ya kuwanukuu kwenye vyombo vyenu vya habari, isipokuwa kama mmekubaliana hivyo toka mwanzo.
Aidha, Idara yetu ya Uhusiano wa Umma na Itifaki ipo Benki Kuu kwa ajili yenu, hivyo itumieni vya kutosha kila wakati mnapotaka kupata taarifa mbalimbali kutoka Benki Kuu.
Benki Kuu inaridhika na jinsi waandishi wa habari na vyombo vya habari vinavyotoa ushirikiano mara nyingi inapokuwa na uhitaji. Aidha, tunafurahi tunapopata miito yenu ya kushiriki katika vipindi vyenu na kutoa ufafanuzi, ili umma wa Watanzania uelewe masuala mbalimbali yanayohusu Benki Kuu.
Ameongeza kuwa katika semina hii kumekuwa na ushiriki mkubwa wa radio za kijamii na televisheni. Hili ni jambo muhimu sana ili kuhakikisha taarifa za Benki Kuu, ambazo zinawagusa wananchi wote zinawafikia wote huko waliko na waandishi wao ambao wameelimika.
“Hata hivyo, idadi ya washiriki bado ni ndogo na elimu zaidi inahitajika. Benki Kuu itaendelea kutumia mbinu mbalimbali ili kuwafikia na kuwaelimisha,” Amesema Vick Msina.
Akifafanua zaidi amesema pamoja na mambo mengi ambayo mmejifunza, napenda mtusaidie kueneza ujumbe huu kwa wananchi kama sehemu ya kuhakikisha sekta ya fedha nchini inaimarika, inachangia zaidi katika uchumi wa nchi yetu na kuzidi kuleta maendeleo .
Amewataka waandishi wa habari kuhamasisha wananchi wanaochukua mikopo katika benki na taasisi za fedha mbalimbali kuhakikisha wanatumia fedha wanazokopa kwa malengo tarajiwa na kurejesha mikopo hiyo kwa wakati kwani Kwa kufanya hivyo, watakuwa wanajijengea jina zuri la kukopesheka, na hivyo kuweza kupata mikopo zaidi na pengine kwa riba nafuu zaidi.
Hii itawasaidia wao katika shughuli zao za kiuchumi, kuweka vizuri mizania ya mikopo ya benki na taasisi husika na kufanya ziweze kukopesha watu wengi zaidi. Aidha, wananchi wanapaswa kukumbuka kwamba, kwa sasa, taarifa zao zote za mikopo zinapatikana, hivyo wasipokuwa waaminifu, watajifungia nafasi ya kupata mikopo kwenye taasisi zingine.
Bi.Vick Msina ameongeza kuwa bado wananchi wengi hawazingatii elimu ya utunzaji mzuri wa noti zetu ili zidumu kwa muda mrefu zaidi na kupunguza gharama kwa serikali kuchapisha fedha zingine.
“Watu wanakunjakunja hovyo noti au kuzishika wakiwa na unyevunyevu au damu hali ambayo inapunguza kwa kiasi kikubwa uhai wa fedha hizo na kulazimisha serikali kuingiza gharama za kutengeneza zingine,” Amesema Bi. Vick Msina
Aidha amesema matumaini yetu ni kwamba kupitia elimu mliyoipata, mtakuwa mabalozi wetu kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutunza fedha katika hali nzuri.
Kama alivyosema Naibu Gavana wakati anafungua semina hii. Ni wajibu wenu kuhamasisha wananchi kujihusisha na shughuli za ujenzi wa taifa; kutangaza kazi mbalimbali, zikiwemo za ubunifu ambazo wananchi wanafanya na kuchangia maendeleo ya taifa pamoja na fursa mbalimbali ambazo, ama zimeendelezwa kidogo, au hazijaendelezwa kabisa, ili kuvutia wawekezaji kuziendeleza na kwa jinsi hiyo kuchangia maendeleo ya taifa.
Mtandao mliojenga miongoni mwenu pamoja na maafisa wa Benki Kuu utumike kwa ajili ya kukuza Habari ya biashara, uchumi na fedha kwa kushirikishana uzoefu mbalimbali mnaopitia katika kazi kwa lengo la kuboresha.
Baada ya kukaa hapa Benki Kuu Mbeya mkijifunza, endapo mtarudi nyumbani na kutopitia mliyojifunza hapa, au kutumia elimu mliyopata kuboresha kazi zenu, mtakuwa mmepoteza siku tano muhimu kwa maendeleo yenu.
Amemalizia kwa kusema Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kushirkiana na vyombo vya Habari mbalimbali ambavyo ni kiungo muhimu katika kuwafikia wananchi, na kuchukua taarifa kwa wananchi ziweze kutufikia sisi kama mrejesho.
Aidha, kama wawakilishi wa BenkiKuu katikasemina hii tumesikia na kupokea mapendekezo na maoni yenu mbalimbali kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati yenu na Benki Kuu na kuahidi kwamba tutayafanyia kazi.