Meneja Idara ya Kilimo wa Kampuni ya Mkulazi, Mhandisi Flavian Reginald (kushoto) akimpa maelezo kuhusu maendeleo ya Shamba la miwa Mkulazi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, aliyetembelea mradi huo mwishoni mwa wiki.
Mkandarasi Mkuu wa ujenzi wa kiwanda cha sukari Mbigiri, Vijey Kumar akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa kiwanda hicho mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi huo mwishoni mwa wiki. Mhe.Waziri ameitaka Kampuni inayojenga kiwanda hicho kukamilisha ujenzi ndani ya muda kutokana na umuhimu wa kiwanda hicho kwa wananchi wa Wilaya ya Kilombero na maeneo jirani.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kushoto) akizungumza na watendaji mbalimbali wakati alipotembelea mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mhe. Alhaji Majid Mwanga.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kukagua mradi wa kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri mkoani Morogoro, mwishoni mwa wiki, ambapo alimwagiza mkandarasi mkuu kuongeza kasi na kumaliza mradi kwa wakati, katika ziara hiyo aliambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Profesa Jamal Katundu.