…………………………………………………………
Na.Mwandishi Wetu,DODOMA
SERIKALI imewaasa vijana wasomi nchini kuwa wazalendo katika kujenga uchumi kwakuwa na ajenda ya pamoja katika kukabiliana na changamoto za ajira.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Katiba na Sheria George Simbachawene,wakati wa maombi ya Kitaifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Kingdom Leadership Network iliyoshirikisha Vijana mbaalimbali nchini lengo nikuwapa elimu mbalimbali ikiwemo kujiinua kiuchumi na Taifa kwa ujumla.
Simbachawene amesema kuwa ili taifa liweze kuwa na uchumi imara vijana wasomi wanatakiwa wawe mstari wa mbele katika kuinua uchumi pamoja na kutatua changamoto za ajira zilizopo.
“Sasa hivi kumekuwa na vijana wasomi wengi na wengine bado hawana ajira lakini naamini kupitia makongamano haya ni fursa zitaweza kuwatoa walipo na kujiajiri wenyewe badala yakutegemea kuajiriwa,”amesema
Amesema katika kongamano hilo amejifunza masuala ya uzalendo kuwa mbele hivyo ni muhimu vijana kutumia fursa za makongamano mbalimbali ili kuweza kukaa pamoja kujadili changamoto zao hasa ya ajira .
“Forum hii ya Kingdom Leadership Network KLN imekuwa na kitu Cha tofauti kwani nimefurahia imeweza kuwakutanisha vijana wengi ukiangalia hivi Sasa tuna vijana wengi na tunachangamoto kubwa ya ajira hivyo kupitia mafunzo waliyopata wataenda kuwaelimisha wenzao katika suala nzima la ajira”, amesema Mhe.Simbachawene
Kwa Upande wake Mchungaji Dk.Barnabas Mtokambali ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Kanisa Assemblies of God (TAG) amesema kuwa amefurahi kuona maombi kwa ajili ya Taifa kwani ni muhimu kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi na Viongozi wake huku akitoa wito kwa Serikali kushiriki kikamilifu katika maombi hayo Mwakani.
Naye Askofu wa Kanisa la Waadiventista sabato Tanzania Walwa Malekana ,amesema maudhui ya Kongamano hilo limemvutia kutokana na mada mbalimbali zilizotolewa hasa vijana kuwa wabunifu ili kutatua matatizo yao pamoja na kwakutiwa Moyo kuhusu masuala ya ukosefu wa ajira.
”Vijana ajira zipo mashambani ,migodini hivyo ni ubunifu tu na uthubutu wa kufanya ”.