ya Wakurugenzi ya kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd, Mehboob Karmali akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kampuni hiyoiliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Viongozi wa kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd, wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wao wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kampuni hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Wakati Watanzania wakisherehekea Miaka 60 ya uhuru tareh 9-12-2021 siku ambayo Bendera ya mkoloni ilishushwa na kupandishwa Bendera ya Tanganyika katika mlima Kilimanjaro
Tarehe kama hiyo mwezi wa pili mwaka 2007 aliyekuwa Mkurugenzi wa FK motors, Mehboob Karmali aliamua kuanzisha kampuni ya uuzaji wa Magari na mitambo ya kutengenezea barabara GF Trucks & Equipment’s
Akizungumza wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kampuni hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa GF, Mehboob Karmali alisema haikuwa kazi rahisi kufika hapo walipo kwani jitihada binafsi kwa kushirikiana na wafanyakazi ndio zimewafikisha tulipo
Kwa mara ya kwanza ilikua ngumu Sokoni kutambulisha bidhaa za kichini yaani magari ya FAW ambao sisi ndio wauzaji wakubwa wa magari hayo nchin
Pia tunawashuku wateja wetu wakubwa kipindi hicho Bonite ,Asas na Azam ambao kwa miaka hiyo ndio walikua wateja wetu wakubwa
Nae Mkurugenzi wa kampuni hiyo alisema kuaminiwa na kuongoza kamuni yenye wafanyakazi zaid ya 200 ni kazi ngumu lakini anashukuru Mungu kutokana na umoja uliopo baina ya wafanyakazi wateja na uongozi wa kampuni hiyo kazi zinaendelea.
Akikumbuka jinsi walivyoliteka soko la bidhaa hizo za FAW na baadae XCMG nchini ilikua hawana namna kuna wakati ilibidi wapiti kwa wateja wakubwa na kuwaomba wachukue magari hayo na mitambo watumie kwa kipindi cha miezi sita kama hayataharibika basi watafaya malipo na ndio mbinu iliwasaidia kufanikiwa lakini ilikua ni kama kujilipua Pia Gf ni wauzaji wa Mitamboy a XCMG,WEICHAN ,HONY YANG na FAW
Kwa jitihada hizo siku hadi siku kampuni iliendelea kukua na kujitangaza siku hadi siku na leo tunajivunia kuanzisha kiwanda cha kuunganisha magari kilichopo Kibaha mkoani Pwani ni GF- Vehicle Assembly Ltd haya yoote ni matunda ya miaka 15 ya GF
Kwa upande wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambae ni mhasisi Salum Issa ambae aliibuka mmoja ya wafanyakazi bora alisema kikubwa ni kumshukuru mungu kwani ukaribu wa viongozi wao kwa wafanyakazi ndio unapelekea wao kujituma na kujitolea pale inapobidi kwa faida ya wafanyakazi na kampuni pia Maswala ya matatizo popote huwa hayakosi muhimu ni kuvumiliana na kuchapa kazi
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya kampuni ya GF Trucks & Equipment’s Ltd, Mehboob Karmali (katikat) akiwaongoza wakurugenzi wenza kukata keki wakati wa hafla ya kutimiza miaka 15 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam.