………………………
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
Viongozi wakiwemo maafisa watendaji wa vijiji,kata ,walinzi wa amani wameaswa kusimamia haki katika utatuzi wa migogoro mbalimbali ndani ya jamii ili kulinda amani .
Akitoa Rai hiyo, katika mafunzo ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani kupitia mradi wa jenga amani yetu, na kuandaliwa na kituo Cha sheria na haki za binadamu ( LHRC) ), huko Ikwiriri,Rufiji, Pwani Kamishna msaidizi wa polisi,mkoa wa kipolisi Rufiji,oparesheni ofisa Mushi, akimwakilisha kamanda wa polisi, alisema watumishi wa umma na walinzi wa amani watende haki kulinda amani.
Alieleza chanzo cha migogoro ni kukosekana kwa haki katika migogoro inayotokea katika jamii ikiwemo wafugaji na wakulima,ndani ya familia,mirathi,ardhi migogoro hii ukiifuatilia Sana inatengenezwa na baadhi ya viongozi wasio waadilifu kwa kukosekana haki.
“Mradi huu ni wa msingi na uendelezwe, amani ni tunda la haki paispo Kuwa na haki hakuna amani,ukitenda haki umeleta amani,ukichukua mayai 30 wakawa watoto watano,ukampa mtoto mkubwa agawie wenzake atachukua kumi yake ndio agawie wenzie mengine hapo ndipo amani huanza kutoweka”
Nae Ally Seif kutoka mradi wa Jenga Amani Yetu alisema wanatoa elimu na kufanya mikutano kukutanisha wadau kwa kushirikiana na shirika la Search for Common Ground na ZLC kwa ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya.
Alieleza ,katika mafunzo hayo wamewakutanisha Jeshi la polisi, waandishi wa habari na asasi za kiraia.
“Tumegundua migogoro mikubwa mkoa wa Pwani Ni ardhi,ndoa na mirathi ugawanywaji wa Mali za marehemu,wanatoa Suluhu wakiwa hawana mbinu za kutatua migogoro hiyo hivyo tumetoa mafunzo ili kuweza kukabiliana na migogoro hiyo.”alifafanua Seif.
Seif alisema, sio kazi ya polisi ama waandishi wa habari, watendaji wa vijiji,kata ama Serikali kulinda amani pekee badala yake kila mwanajamii anawajibu ananufaika na amani, pia ni wahanga wakati amani ikipotea .
“Tumegundua migogoro hiyo wakulima na wafugaji,ndoa,ardhi, mirathi ni mingi,wanaotoa Suluhu wanakuwa na Uelewa na mbinu haba,kutofikia Sheria lengwa, wameeleweshana mbinu Bora kuweza kufikia sheria na Suluhu ya amani ili kutatua migogoro inayojitokeza.”
Agnes wela kutoka kituo Cha kulelea watoto yatima Ikwiriri aliishukuru mradi wa Jenga Amani Yetu, kwa kuweza kupata mafunzo ya mbinu na namna ya kuttaua migogoro kwa njia ya amani.