Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Martin Mwambene akizungumza na waandishi wa habari wakati alipoelezea kurejea katika hali ya kawaida kwa upatikanaji wa umeme baada ya kukamilika kwa kazi ya kuboresha mitambo ya kuchakata gesi Songosongo Kilwa mkoani Lindi.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Martin Mwambene wakati alipoelezea kurejea katika hali ya kawaida kwa upatikanaji wa umeme baada ya kukamilika kwa kazi ya kuboresha mitambo ya kuchakata gesi Songosongo Kilwa mkoani Lindi.
Baadhi ya mitambo ya Kinerezi II jijini Dar es Salaam inavyoonekana.
………………………………
SHIRIKA la Umeme Tanzania(TANESCO) limewaomba radhi wananchi kwa usumbufu walioupata katika kipindi hicho cha siku kumi, kutokana na maboresho yaliyofanyika na yanayoendelea kufanywa na Shirika hilo ambayo yanatarajiwa kuleta tija na kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme nchini.
Amesema upatikanaji wa umeme nchini kwa sasa umerejea katika hali ya kawaida na hiyo ni baada ya kukamilika maboresho ya mitambo ya uzalishaji wa gesi katika visima vya Songosongo.
Hayo yamesemwa na Msemaji wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Bw. Martin Mwambene wakati akzungumza na waandishi wa habari leo kkatika mitambo ya kufua umeme ya Kinyerezi II Jijini Dar es Salaam.
Bw. Mwambeme amesema kutokana na hatua hiyo, zile siku kumi za upungufu wa umeme ambazo TANESCO ilizitangaza na kuhusisha baadhi ya maeneo kukosa umeme kwa nyakati fulani zimehitimishwa rasmi.
Awali TANESCO iliwatangazia wananchi kuwepo kwa upungufu wa umeme huo katika baadhi ya maeneo kwa kipindi cha siku kumi hali iliyopelekea ukosefu wa nishati hiyo kwa wastani wa siku mbili hadi tatu katika baadhi ya maeneo nchini.
“Niwataarifu wananchi kuwa upatikanaji wa umeme umerejea kawaida kama awali hii imefuatia kazi nzuri ya uboreshaji wa mitambo ya uzalishaji gesi Songosongo iliyokuwa inaendelea katika visima vya Songgas sambamba na baadhi ya mitambo yetu ili kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme” amesema Mwambene
Awali shirika hilo kupitia kwa Mtendaji wake Mkuu Maharage Chande lilisema kuwa katika jitihada hizo za kuongeza kiwango cha upatikanaji wa umeme TANESCO itaboresha pia na kufanyia matengenezo ambayo bado yanaendelea kuboresho katika vituo vyake viwili kikiwemo cha Kinyerezi I kitakachozalisha Megawati 185 ambazo zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.