Naibu waziri wa ofisi ya RaisTawala za mikoa na serikali za mitaa ,David Silinde akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha leo.(Happy Lazaro).
……………………..
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa
David Silinde ameeleza kuwa serikali ya Tanzania imekuwa ya mfano wa kuigwa ndani ya wanachama jumuiya ya Afrika mashariki kwa kuweza
kugatua madaraka kwa Bajeti zake kuanzia ngazi za chini katika
serikali za mitaa.
Silinde ameyasema hayo Leo jijini Arusha wakati wa Mkutano wa Jumuiya ya Afrika
mashariki ya serikali za mitaa (EALGA) iliyofanyika jijini Arusha
ambapo ameeleza kwamba nchi wanachama wa jumuiya hiyo kwa siku tatu
watajadili kuona ni kwa kiwango gani wamefanikiwa kuweza kuisaidia
jamii kuongeza wigo wa maendeleo katika Bajeti zao.
Aidha amesema kuwa, hivi sasa hapa nchini kumekuwepo mjadala mrefu wa
kushirikisha wadau mbalimbali katika kuandaa bajeti yetu kutoka
makundi mbali mbali kuanzia sekta binafsi na ngazi za serikali za
mitaa kuanzia WDC hili linajenga wigo wa kuishirikisha jamii kufikia
malengo ya kidemokrasia.
“Tanzania imekuwa nchi ya kupigiwa mfano katika suala zima la ugatuaji
wa madaraka ndio maana jumuiya hii ya serikali za mitaa kwa nchi
wanachama wa Afrika mashariki imeona ni vyema kujadili kwa kina suala
hilo kuongeza wigo wa Demokrasia ya kushirikisha wadau wa maendeleo na
jamii zetu”amesema.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Christophe Bazivamo amesema kwamba ipo haja kuishirikisha jamii nzima ya wanajumuiya hiyo kuweza kuona jamii ya wanaafrika mashariki wakiongeza wigo wa kushiriki katika maandalizi ya bajeti zetu kutoa
maoni yao.
Amesema kuwa, serikali zetu kwa kushirikiana na jumuiya hiyo
zimekusudia kuungana na kuchagua kupitia kifungu cha saba kwa
kushirikiana jamii na sekta binafsi katika kukuza maendeleo ya Pamoja
kwa washika dau wote.
Ameongeza kuwa, serikali za mitaa ndio ufunguo wa kuifikia jamii nzima
kuweza kushiriki kwa Pamoja katika kuuandaa sheria na bajeti
zitakazosaidia kuwezesha jamii kuweza kupiga hatua za kimaendeleo
ndani ya wananchi wa jumiya ya Afrika mashariki.
“Huu ndio msingi mkubwa wa kuwa na jamii inayoshirikishwa tumeona
Tanzania imefanikiwa sana katika Ugatuzi wa madaraka hivyo tupo Pamoja
katika kufikia malengo ya jumiya kuweza kusaidia serikali za nchi
wanachama kufikia kuwezesha na kuibua miradi ya maendeleo kuanzia
ngazi za chini,”amesema Silinde.
Naye Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,John Pima ameeleza kwamba mambo yatakayojadili ni suala la ugatuzi wa madaraka ambao jiji la Arusha
linautekeleza kwa kuwepo na uchaguzi wa kidemokrasia kuanzia ngazi za
chini Pamoja utawala bora.
Pima amesema kuwa, shirikisho hilo lilianzia mkoani Arusha miaka ya 2002
hivyo sasa unaona jiji letu kwa mfano shule zetu zina Bodi za shule
hizi ni ugatuzi wa madaraka zamani utaona vitu kama hivyo vya shule
vinasimamiwa na wizara ila sasa ni wananchi wenye ndio wanasimamia
uendeshaji.
Mwisho