Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO , Maharage Chande akizungumza na waandishi wa habari katika kituo cha kupozea umeme cha Kunduchi mara baada ya kukagua ufungaji wa tfansfomer unaoendelea kituoni hapo.
Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kinondoni kaskazini,Regina Mvungi akishukuru Shirika na Serikali kwa ujumla kwa kufunga Transfoma hiyo kwa sababu itapunguza sana changamoto ya kukatika umeme kwa wateja kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO , Maharage Chande
Abubakar Issa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji TANESCO akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika kituo hicho.
Picha mbalimbali zikionesha mafundi wa TANESCO wakiendelea na ufungaji wa Transfoma hiyo mpya itakayosaidia kugunguza tatizo la kukatikakatika kwa umeme jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika Shirika la Umeme Tanzania TANESCO , Maharage Chande amesema Februari 2 mwaka huu wanatarajia kuanza kuiwasha Transforma mpya inayofungwa katika kituo cha kupooza umeme cha Kunduchi baada ya kukamilisha matengenezo yake.
Akizungumza leo Januari 31,2022,baada ya kutembelea kituo hicho amesema Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),limefunga Transfoma hiyo ili kuondoa baadhi ya changamoto zilizokuwa zinajitokeza kwa wateja kupata usumbufu wa kukatikakatika kwa umeme.
Amesema Tranfoma hiyo yenye thamani ya Sh 2.8 Bilioni itasaidia sana katika kipindi cha siku 10 ambazo kutakuwa na upungufu wa umeme na kusababisha baadhi ya maeneo kuwa na mgao wa umeme kutokana na marekebisho ambayo yatakuwa yakiendelea katika kipindi hicho.