Wasomi kutoka jamii ya wafugaji waishio wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wakizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Selina Mungaya ambaye ni Msomi chuo kikuu Mzumbe akizungumza na waandidhi wa habari jijini Dar es salaam kueleza namna msimamo wao ulivyo katika Wilaya ya Ngorongoro
Msomi kutoka Chuo Kikuu SUA Megoliki Meng’oru akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es salaam
…………………………..
NA MUSSA KHALID
Wasomi kutoka jamii ya wafugaji waishio wilayani Ngorongoro mkoani Arusha wameiomba serikali iweke meza ya pamoja ya mazungumzo na jamii ya wafugaji na wahifadhi wa hifadhi ya Ngorongoro juu ya changamoto wanayokumbana nayo inayotokana na mgogoro wa ardhi wilayani humo.
Wakizungumza leo na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam wasomi hao jamii ya Masai kutoka Wilaya ya Ngorongoro wamesema wamekuwa wakipitia kadhia ya kutakiwa kuhama katika eneo hilo wakidaiwa kuwa wamekuwa wakiharibu hifadhi hiyo ya utalii wakidai ni tofauti na malengo ya kuanzishwa kwa hifadhi hiyo kwani ililenga kuendeleza Uhifadhi, Utalii na kuendeleza watu wanaoishi ndani ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro.
Aidha wamedai kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ikifanya Kampeni ya hila dhidi ya wakazi hao jamii ya Masai wanaoishi ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa lengo kufanya waweze kutolewa ndani ya hifadhi pamoja na kuweka mazingira yasiovumulika binadamu kuweza kuishi.
Ezekiel Ole Mangi ni Msomi jamii ya wafugaji pamoja na Laata Mekusi ambaye ni Msomi Chuo Kikuu Mzumbe wameiomba Serikali itambue kuwa eneo la kilometa za mraba 1,500 linalodaiwa kuwa litakuwa pori tengefu lina maslahi na wananchi kwani ndipo vilipo vyanzo vya maji na malisho kwa ajili ya mifugo na itambulike kuwa ufugaji ndio rasilimali pekee ya wananchi wa loliondo
‘Tunaisihi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na serikali kukaa meza moja na na wakazi wa Ngorongoro inapokuja haja ya kutafuta namna bora ya kuboresha hifadhi kama kampeni ya upandaji wa miti na wenyeji wakati wote wapo tayari kushiriki’wamesema wasomi hao
Vilevile Msomi chuo kikuu Cha SUA Megoliki Meng’oru pamoja na Selina Mungaya ambaye ni Msomi chuo kikuu Mzumbe wameishauri Serikali iwashirikishe wadau wote wa Loliondo katika mchakato wa kutatua mgogoro huo na kuzingatia yafuatayo
Wameisihi Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Kwamba wanachi hawajawahi kuwa tatizo kwa wanyama wala uhifadhi kwa ujumla ila ni sera na sheria ambazo zimekuwa ni kindamizi kwa Maisha yao, Hivyo ni wakati muafaka kuandaa mjadala juu ya kurekebisha sera na sheria zilizopitwa na wakati hasa zinazokandamiza utu na kukiuka haki za binadamu
Katika hatua nyingine wasomi hao wamebainisha athari wanazozipata kutokana na mgogoro huo ikiwemo janga la njaa, mlipuko wa magonjwa yanayoambukiza na yasiyoambukiza yanayotokana na ukosefu wa lishe bora ambapo mgogoro huo umepelekea wakazi hao kushindwa kufanya shughuli za uzalishaji.
Aidha wasomi hao wamesema kuwa kutekeleza dhana inayofikiriwa na wahifadhi ya kuunda Ngorongoro mpya kuwaondoa jamii ya wafugaji katika hifadhi hiyo itapoteza uhalisia wa uanzishwaji wa hifadhi ya Ngorongoro.
Ikumbukwe kuwa Jan 25 mwaka Mratibu wa Kitaifa wa THRDC Onesmo Olengurumwa wakati akizungumza na wanahabari akitoa taarifa ya hali ya utetezi wa Haki za Binadamu katika migogoro ya Ardhi Wilayani Ngorongoro alimuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluh Hassan kuwapa nafasi na kuwasikiliza wananchi wa Loliondo ili kusikia hoja zao na hatimaye azifanyie kazi ili mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.
Pia aliiomba Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko ya wananchi na kuchukua hatua stahiki ili kuzuia ukiukwaji wa haki za binadamu Wilayani Ngorongoro.