Meneja Mawasiliano wa Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA Lulu Kansary akiwaeleza vijana wa kijiji Kijiji Cha Kauzeni Kata ya Kibuta Wilaya ya Kisarawe lengo la kutoa mafunzo kwa njia ya mdahalo kuhusu masuala ya unyanyapaa,ubaguzi na ukatili wa kijinsia pamoja na mapambana ya kujikingia na ugonjwa wa UVIKO-19.
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wilaya ya Kisarawe Mwandili Rangi (aliyevaa koti jeusi la suti) akitolea ufafanuzi kuhusu malalamiko mbalimbali ya kufanyiwa ukatili wa kijinsi katika maeneo yao na familia zao.
Kijana Suleiman Issa akieleza namna anavyofahamu kuhusu ukatili
Baadhi ya vijana ambao wameshiriki katika mdahalo huo wakisikiliza kwa makini.
……………………..
NA MUSSA KHALID,KISARAWE PWANI
Matukio ya vitendo vya kikatili vikiwemo vya unyanyapaa na ubaguzi wa kijinsia yametajwa kuendelea kujitokeza katika jamii kutokana na kutokuwa na elimu ya wapi wapeleke malalamiko yao pindi wanapokumbana na vitendo.
Hayo yamebainika katika ziara ya Baraza la Taifa la watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi NACOPHA wakitekeleza mradi wa Shirika la Ukimwi Duniani-UNAIDS walipotembelea Kijiji Cha Kauzeni Kata ya Kibuta Wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kutoa mafunzo kwa njia ya mdahalo kuhusu masuala ya unyanyapaa,ubaguzi na ukatili wa kijinsia pamoja na mapambana ya kujikingia na ugonjwa wa UVIKO-19.
Akizunguma Katika mjadala wa pamoja vijana mbalimbali Katika Kijiji hicho Meneja Mawasiliano wa NACOPHA Lulu Kansary amewapa elimu vijana hao kuhusu katili mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ukatili wa Kingono,kiuchumi pamoja ukatili wa uhuru wa kisaikolojia.
“Maana ya ukatili ni kufanyiwa vitendo bila ya ridhaa ya mwenyewe kama mfano kama ambavyo mumesema kuna changamoto mbalimbali za ukatili mwingine unaweza kuitwa mwizi kumbe sio mwizi hivyo inakuwa umekatiliwa kisaikolojia au pia ukatili wa haki ya msingi ya kutokujieleza.”amesema Lulu
Kwa upande wao baadhi ya vijana ambao wameshiriki katika mdahalo akiwemo Suleiman Issa Pamoja Lukinga Mohamed wamesema wamekuwa wakikumbana na vitendo vya kikatili kwenye familia zao pamoja na kwenye shughuli zao za kujipatia kipato.
Lukinga ameeleza uelewa wake kuhusiana na ukatili hasa wa unyanyasaji wa kijinsia kuwa ni Pamoja vitendo vya ubakaji,ulawiti na kuwanyanyasa watu wenye changamoto za ulemavu.
“Huwa tunakumbana na changamoto tunapopeleka kesi serikali za chini huwa haitatuliwi kwa haraka au unakuta Mtu aliyefanya kitendo cha kikatili anakuwa no mwenye uwezo wa kifedha hivyo anasababisah kesi kutosikiliza Kwa kutokuwa na mwendelezo”wamesema wnanachi
Afisa Ustawi wa Jamii kutoka Wilaya ya Kisarawe Mwandili Rangi amewataka Wananchi hao kuhakikisha wanatoa taarifa ya Matukio ya kikatili yanayojitokeza kwenye maeneo yao Ili utaratibu uweze kufatwa kwa kuchukuliwa hatua watu wanaotuhumiwa.
Naye Mwenyekiti wa Konga Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Mariam Kologombe amesema fursa ya NACOPHA kwenda katika Kijiji hicho imesaidia wananchi kuwa na uelewa wa masuala mbalimbali ya ukatili.
“Watu wengi unakuta tunafanyiwa ukatili bila ya kujua sababu hatuna elimu jambo ambalo linafanya Matukio kuendela kukithiri kila kukicha hivyo ujio wa NACOPHA kuja ni sehemu sahihi ya kuisaidia Jamii kuweza kujikomboa na vitendo hivyo kwa kuufahamu nna ya kutoa taarifa sehemu husika”amesema Bi Mariamu
Hata hivyo Kaimu Afisa Maendeleo Wilaya ya Kisarawe Dalidali Rashidi ametoa wito kwa watu wote wanaokumbana na vitendo vya kikatili kutoa taarifa kwa wakati kuanzia wanapoona dalili za vitendo vya ukatili.
Mradi huo ambao unatekelezwa na NACOPHA kwa kuwezeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na vita Dhidi ya Virusi vya VVU na UKIMWI umefanyika katika mikoa mitano nchini ukiwemo WA Pwani katika Wilaya ya Kisarawe na hiyo nikutokana na kuwa matukio mengi ya ukatili kwa mabinti wadogo kuolewa wakiwa na umri mdogo