Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akizungumza baada ya mapokezi Chanjo dhidi ya UVIKO-19 Aina ya Sinopham ambayo imefanyika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian akizungumza na waaandishi wa habari katika hafla ya mapokezi ya Chanjo dhidi ya UVIKO-19 Aina ya Sinopham ambayo imefanyika katika uwanja wa Kimataifa wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
…………………….
Serikali imepokea Chanjo aina ya Sinopharm kwa ufadhili wa Serikali ya China yenye jumla dozi 800000 ambazo zitatumika kuchanja wananchi 400,000.
Hayo yamejiri leo jijini Dar es salaam katika hafla ya mapokezi Chanjo dhidi ya UVIKO-19 Aina ya Sinopham ambayo imefanyika katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa mapokezi wa Chanjo hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ameipongeza Serikali China Kwa kuwezesha upatikanaji wa Chanjo hiyo ikiwa ni ya awamu ya Pili kutoka katika Serikali hiyo kwani awamu ya Kwanza walipokea jumla ya dozi 500,000 ambazo zilitumika kuchanja wananchi 250,000.
‘Mapokezi ya Chanjo za leo yanafanya jumla ya chanjo tulizopea nchini tangu tuanze kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 hadi sasa kuwa dozi 8,821,210 zikijumuisha (Sinopham,Janssen,Modema na Pfizere) ambazo zinatosha kuchanja Jumla ya Watanzania 5,082,280’amesema Waziri Ummy
Waziri Ummy amesema kwa mujibu wa Takimu mpaka kufika Januari 23 mwaka huu Juma ya watu 349,641,119 wamethibitika kuwa na maambukizi na watu 5,592,266 wamepoteza maisha Duniani kote huku kwa nchini Tanzania kukiwa na jmla ya wa watu 33,000 wamethibika kuwa na maambukizi na 781 wamepoteza maisha.
Kuhusu chanjo ya UVIKO-19 Waziri Ummy amesema imeshuhudiwa kuwa ufanisi mkubwa kwakupunguza makali ya ugonjwa ikiwemo kulazwa na kifo endpo mhusika atakamilisha idadi ya dozi aliyoshauriwa hapa nchini.
Amesema kuwa serikali imekuwa ikifuatilia taarif za kuchanjwa miongoni mwa wagonjwa katika vituo vya huduma.
‘Nachukua fursa hii kuwaagiza viongozi wa serikali wa ngazi zote katika Mikoa ,wilaya,Halmashauri,Kata,Vijiji kutoa Ushirikiano wa wa hali juu ili kuhakikisha kuwa wananchi wanahimizwa kwenda kwenye vituo vya afya ili wakapate elimu kuhusu umuhimu wa chnjo na kisha Wachanje’amesema Ummy