Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara ( TanTrade ) Bi.Latifa Khamis akishuhudia utiaji Saini uuzaji wa Nyama ya Mbuzi Kati ya Kampuni ya Borema Affairs ya Tanzania na kampuni ya DYLYK FOR FOOD TRADE ya Doha- Qatar.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) kwa mara nyingine imefanikiwa kuwaunganisha wafanyabiashara wa ndani na Masoko ya nje ya nchi .
Leo tarehe 23Januari,2022 Kampuni ya *Borema Affairs* wamefanikiwa kusafirisha Tani mbili za nyama ya Mbuzi ikiwa ni sehemu ya mkataba wa kusafirisha Tani 120 ( Kilo 120,000) za nyama ya Mbuzi kwa kila mwezi kwenda Doha nchini Qatar.
Fursa Hiyo inatokana na Mkataba wa kibiashara uliosainiwa Kati ya Kampuni ya *Borema Affairs na kampuni ya DLYLK for Food Trade* iliyopo *Doha- Qatar*.
Mkataba huo ulisainiwa Mnamo tarehe 22 Disemba,2021 na ulishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa *TanTrade Bi . Latifa Khamis*.
Mkurugenzi wa Borema Affairs *Bw.Thabit Mlangi* ametumia nafasi ameishukuru Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania ( TanTrade ) kwa kufanikiwa kumuunganisha na soko lenye uhakika huku akitoa wito kwa wafanyabiashara na wafugaji nchini kuendelea kuitumia Tantrade katika kutafuta masoko ya nje ya nchi .
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade ambaye ni Meneja wa Utafiti na Mipango *Bw.John Fwalo* _amempongeza Bwana Thabit kwa kufanikisha mkataba huo kwa wakati na kutoa wito kwa wafanyabiashara wengine kuendelea kutumia fursa za kibiashara zinazopatikana TanTrade zenye tija na kufuata taratibu na sheria za nchi_.
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TanTrade) pamoja na mambo mengine ina jukumu la kusimamia ,kuratibu na kuendeleza Biashara za ndani na nje ya nchi .