RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifanya mazoezi ya viungo katika viwanja vya Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma, kabla ya kuaza kwa Matembezi ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria na( Kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma na (kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson , Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, wakiwa na Viongozi wengine wa Serikali na Mahkama.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa katika matembezi ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania inayofanyika Jijini Dodoma katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Hamis Juma na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla na (kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe Dkt. Tulia Ackson, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Anthony Mtaka, wakishiriki katika matembezi hayo yalioazia Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma na kumalizika katika viwanja vya Nyerere Square Dodoma
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifanya mazoezi baada ya kumaliza matembezi ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania yalioazia katika Kituo Jumuisho cha Utoaji Haki na kumalizia katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma na (kushoto kwa Rais) Jaji Mkuu wa Tanzania Prof Ibrahim Hamis Juma na Kaimu Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe.Khamis Ramadhan Abdalla na (kulia kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.George Boniface Simbachawene.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akitembelea maonesho ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania, katika banda la Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) akipata maelezo kutoka kwa Afisa Mradi Bi. Asha Hassan Komba na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe.Prof Ibrahim Hamis Juma, maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi akitembelea banda la maonesho la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Huduma za Sheria.Bw.Stanislavs Kagisa na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.George Boniface Simbachawene.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk,Hussein Ali Mwinyi akitembelea banda la maonesho la Wizara ya Katiba na Sheria akipata maelezo kutoka kwa Dr.Anne Malipula na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wakati wa ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania yanayofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipandika bendera ya Mahkama Kuu Tanzania katika hafla ya Ufunguzi wa Wiki ya Sheria iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma leo 23-1-2022, na (kushoto kwa Rais) Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mhe.Dkt. Tulia Ackson.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiondoa kipazia kuashiria kuizindua Nembo ya Mahkama Kuu Tanzania wakati wa hafla ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma leo 23-1-2022 akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof.Ibrahim Hamis Juma.
WAGENI waalikwa wakifuatilia hituba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kufungua Wiki ya Sheria Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma
BAADHI ya Waheshimiwa Majaji wa Mahkama Kuu Tanzania wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kufungua Wiki ya Sheria Tanzania iliyofanyika katika viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia katika viwanja vya Nyerere Square wakati wa hafla ya ufunguzi wa Wiki ya Sheria Tanzania, iliyoambatana na Matembezi na maonesho mbalimbali yanayohusiana na Sheria.(Picha na Ikulu)