Benki Kuu ya Tanzania imeshiriki Matembezi ya Uzinduzi wa Wiki ya Sheria mwaka 2022 kuanzia Viwanja vya Mahakama Kuu Dodoma mpaka Viwanja vya Nyerere Square. Matembezi hayo yameongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi.