Watalii kutoka mataifa mbalimbali wanaotembelea Banda la Tanzania kwenye Maonesho ya FITUR 2022 yanayoendelea nchini Hispania wameonesha kuvutiwa na Vivutio vya Utalii ikolojia vinavyosimamiwa na TFS.
Akizungumza na Mwandishi wetu, Mwakilishi wa TFS katika Maonesho hayo Mhifadhi Someni Mteleka amesema amefanya Mazungumzo na Bw.Juan Carlos ambaye ni mtaalamu wa kuandaa miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Hispania ambaye amedhamiria kushirikiana na TFS kuandaa andiko la kuimarisha utangazaji wa Utalii Ikolojia.
Mhifadhi Mteleka amesema wananchi kutoka mataifa mbalimbali wameendelea kutembelea Banda la Tanzania kwenye Maonesho hayo na wengi wameweka nia ya kutembelea Tanzania kwa ajiri ya kujionea Vivutio vya Utalii ikolojia vinavyosimamiwa na TFS.
Maonesho ya kimataifa ya Utalii maarufu kama FITUR 2022 yanaendelea kwa Siku ya nne ambapo mataifa mbalimbali yanashiriki kwa kuonesha Vivutio mbalimbali vya Utalii.