Naibu Waziri Wa Maliasili na Utalii Mary Masanja akizungumza katika maafali ya 19 ya Chuo Cha Taifa cha utalii -NCT yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri Wa Maliasili na Utalii Mary Masanja (kulia) akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo Cha Taifa cha utalii -NCT Dkt Shogo Mlozi (alieyavaa viatu vyekundu kushoto) wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazotengezwa katika chuo Chuo Cha Taifa cha utalii –NCT
……………………..
NA MUSSA KHALID, DAR ES SALAAM
Naibu Waziri Wa Maliasili na utalii Mary Masanja amewataka wahitimu wa vyuo katika ngazi mbalimbali kutumia maalifa wanayoyapata ili kujikimboa katika ombwe la ajira na badala yake kuacha kusubiri ajira za serikali au sekta binafsi.
Naibu Waziri Masanja ameyasema hayo katika maafali ya 19 ya Chuo Cha Taifa cha utalii -NCT yaliyofanyika Jijini Dar es salaam ambapo amesema ni wazi kuwa serikali haiwezi kuajiajiri wahitimu wote hivyo lazima watumie taaluma zao katika kubuni vyanzo vyao vya mapato.
Amesema sekta hiyo kwa sasa imeendelea kukua ikiwa ni pamoja na utalii wa ndani hivyo lazima watumie vyanzo vya ndani katika kutangaza utalii kwani itasaidia si tu kujipatia ajira lakini pia kutangaza vivutio hivyo.
‘Sekta ya utalii inaendelea kuimarika kufuatia athari za janga la UVIKO 19 ambapo kunatokana na jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluh Hassan hivyo niwapongeze kwa hatua hii kwa kuwa mumejikusanyia ujuzi na uzoefu wa kutosha’amesema Naibu Waziri Masanja
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Cha Taifa cha utalii -NCT Dkt Shogo Mlozi amesema chuo hicho kimeendelea kuweka mfumo wa kidigitali lengo ni kuongeza ufanisi kutokana na mabadiliko ya teknolojia.
Nao baadhi ya wahitimu wa chuo hicho wamesema kuwa mfumo wa kuajiajiri ni mzuri kutokana inajenga uwanja mpana wa kuwa na mawazo ya kuleta ubunifu.
Takribani wahitimu 541 wametunukiwa vyeti katika ngazi za stashahada na astashahada kutoka katika kampasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Arusha, Dar es salaam na Mwanza.