Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki yaN NMB, Filbert Mponzi akizungumza na wageni waalikwa kabla ya kusaini mkataba wa makubaliano ya kimkakati na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza ukusanyaji wa mapato sekta ya utalii.
Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akisaini mkataba wa makubaliano ya kimkakati na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kukuza ukusanyaji wa mapato sekta ya utalii.
……………………………………..
Benki ya NMB imesaini makubaliano ya kimkakati na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kushirikiana katika kuimarisha na kukuza ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya utalii visiwani humo kupitia mifumo ya kidijitali.
Makubaliano hayo yamesainiwa leo na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Fatma Mabrouk Khamis.
Kupitia ushirikiano huu, Benki ya NMB itachagiza shughuli za kitalii kupitia;
ambapo itawekeza kwenye mfumo wa kidigitali utakaotumika kufanya makusanyo ya Serikali katika vituo vyote vya utalii Zanzibar
Itasambaza mashine za malipo (POS) kwenye vituo vya makusanyo na vivutio vya utalii. Hii itawawezesha watalii kulipia ada na tozo zote kupitia kadi zao za Mastercard, Visa na UnionPay
Pia itatoa elimu na kuhamasisha watu kuzidi kutembelea vivutio vya kitalii vilivyopo visiwani humo kupitia matamasha na promosheni mbali mbali.