………………….
NA MUSSA KHALID
Wafanyabiashara wa Soko la Mchikichini Karume jijini Dar es salaam wametakiwa kuwa watulivu wakati serikali ikiendea kufanya uchunguzi kwa siku 14 kuhusu chanzo cha Moto ambao umeibuka usiku wa kuamkia leo na kutekekeza mali za wafanyabiashara katika soko hilo
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam Ng’wilabuzu Ludigija wakati akizungumza katika eneo la soko hilo na kusema ajali hiyo ya moto imesababisha hasara za mali zote kwa zaidi ya asilimia 98 zimetekea kwa moto huo.
‘Tumetapa taarifa ya tukio la Moto majira ya saa tisa kuelekea saa 10 juu ya moto mahali hapa hivyo ni pongeze Jeshi la Zimamoto na uokoaji pamoja na Jeshi la Polisi mara tu baada ya kupata taarifa walifika kwa wakati na wakapamba an kuuzima moto licha ya kuwa na changamoto kuwa na mabanda mengi katika soko hili la Mchikichini yamejengwa kwa mbao na maturubali juu lakini wameweza kuukabili’amesema DC Ludigija
Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango wametoa pole kwa wafanyabiashara kwa tukio hilo na kuwaomba wawe watulivu wakati uchunguzi ukiendelea kufanyika.
Ludigija amesema baada ya timu yake ya uchunguzi ambayo itaanza kazi siku ya kesho kufanya kazi ndipo watatoa takwimu ya mali ambazo zimetekekea kwa moto na hasara ambazo zimepatikana.
Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wafanyabiashara na wananchi kujiepusha na maneno ya upotoshaji kuhusu chanzo cha moto huo badala yake wasubiri serikali ndiyo itatoa majibu ya chanzo hicho.