…………………………………..
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC idara ya Organaizesheni na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Dkt. Maudline Syrus Castico akihitimisha ziara yake ya Shina kwa Shina ya siku Mbili (2) Mkoa wa Morogoro katika Wilaya mbili za Kichama Mkoani hapo, wilaya ya Morogoro Mjini na wilaya ya Gairo wakati akizungumza na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro wilaya ya Gairo .
Dkt. Castico amesema Taifa linashuhudia mabadiliko Makubwa ya kiuchumi Kwa Muda mfupi na Mkoa wa Morogoro ni moja ya Mkoa uliofaidika sana Kwa kuwa na Miradi mikubwa ya kiuchumi hasa katika sekta ya Elimu, Afya na Maji ambapo baadhi ya miradi imekamilika na mingine inaendela kumalizika tena Kwa Muda mfupi.
Amesema ni vyema Kwa wanachama na watanzania Kwa ujumla kumtia moyo na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na kazi kubwa anazozifanya.
Dkt. Castico Amewataka Wanachama wote wa Chama Cha Mapinduzi na Viongozi wa Chama kuelekea Uchaguzi wa Chama ndani ya Chama Mwaka huu 2022 Kujipima Mwenye Amefanya nini.
“Kila mtu atapimwa kwa kile alichokifanya ndani ya Chama , Kila mtu Atavuna alicho panda kama ulifanya Mzaha ndani ya Chama utalipwa sawasawa na kazi uliyoifanyia Chama “Amesema Castico
Aidha Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa Morogoro Ndg. Dorothy Mwamsiku amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Samia Kwa Fedha nyingi alizozitoa Kwa miradi ya Maendeleo Mkoani hapo ambazo hazijawahi kutolewa ndani ya Mkoa huo katika awamu zote.
Amesema kama Mwenyekiti amefanya ziara mkoa mzima na kata zote ameshuhudia miradi mingi ikitekelezwa hasa. ukamilishaji wa vyumba vya madarasa Mkoa mzima Huku vituo vya afya na miradi ya Maji ikienda Kwa kasi kubwa.
Amemuhakikishia Dkt. Castico ambaye pia ni Mlezi wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa huo kuwa wataendelea kumuunga Mkono Kwa nguvu zote Mh.Samia na kusema kuwa Wana Morogoro ni chaguo lao na la Mungu katika kuwaletea Maendeleo wa Tanzania.
Katika ziara hiyo ya Shina kwa shina Wilaya ya Gairo Mkoa wa Morogoro Dkt. Castico ameambatana na kamati ya siasa Wilaya ya Gairo na Baraza kuu la jumuiya zote za Chama cha mapinduzi , Viongozi wa Serikali na Kamati ya Ulinzi na usalama wilaya ya Gairo