Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Dkt. Moudline Cyrus Castico Mkuu wa Idara ya Organaizesheni ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM) amesema Uhai wa Chama upo Mashinani ikiwa ni siku ya kwanza ya Ziara ya Siku Mbili Mkoa wa Morogoro ambapo pia ni Mlezi wa Mkoa huo Kichama
Akiwa katika ziara hiyo ya siku Mbili Mkoa wa Morogoro kuanzia tarehe 14 – 15 Jan 2022 leo ikiwa ni Ziara yake ya Kwanza wilaya ya Morogoro Mjini amekutana na Mabalozi wa mashina na kufanya mikutano ya Mashina na kuwakumbusha wananchi na wanachama wa CCM kuwa mwaka Huu 2022 kuna Matukioa makuu Mawili Moja ni Mwaka wa Uchaguzi ndani ya Chama Cha Mapinduzi , Hivyo Watu wajitokeze kwa wingi katika kuwania nafasi mbalimbali ndani ya Chama
Hata hivyo Katibu wa organaizesheni Dkt. Castico amesema wanachama Waandaliwe Kisaikolojia juu ya Uchaguzi ndani ya Chama kwa kuchagua viongozi wenye kutanguliza Mbele Maslahi mapana ya Nchi na Chama Cha Mapindizi (CCM)
Aidha Dkt. Castico Amesisitiza kila mtu Mwenye nia ya Kugombea ajipime na kujiuliza kwanini anaomba nafasi ya Uongozi
“Kila mwenye nia ya kugombea akagombee na vikao vya mapendekezo na uteuzi vikatende Haki kwa kila Mtu bila kujali anacho au hanai“ Amesema Castico .
Dkt. Castico amefafanua Jambo la pili Mwaka 2022 ni Sensa ya Watu na Makazi hivyo kila Mwanachama wa CCM ni vyema akahimiza na kuelimisha jamii kuhusu Sensa itakayofanyika ya Kuhesabu watu ili kupata idadi ya wananchi waliopo katika ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani
Dkt. Amesisitiza Dhamira ya Sensa 2022 ni njema kwa wananchi wa Tanzania kwa sababu itamrahisishia Rais wetu Samia Suluhu Hassan kufikisha Maendeleo kwa wepesi zaidi kwa kujua idadi ya watu na makazi yao kulingana na Geographia husika
“ Hata Mama nyumbani anapika Chakula kwa kujua idadi ya wanafamilia waliopo nyumbni “Amesema Dkt. Castico
Amemaliza kwa kukutana na Kamati ya siasa ya wilaya ya Morogoro Mjini, Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Morogoro Mjini pamoja na Mabaraza ya Jumuiya zote Tatu , Jumuiya ya wazazi wilaya , Jumuiya ya wanawake wilaya (UWT ) na Jumuiya ya Vijana Wilaya (UVCCM)
Katika Kuhitimisha Kikao hicho kizito Dkt. Amewataka viongozi wa Chama na serikali wilaya na Mkoa waheshimu na Kuwatii Mabalozi wa Mashina na kuwatembelea pamoja na kutatua kero za Wananchi Katika kata na Mashinani ili Kuhuisha Uhai Wa Chama Mashinani
_Huu ni Mwendelezo wa Ziara Mashinani hadi kieleweke
Kazi iendelee
imetolewa na
IDARA YA ORGANAIZESHENI CCM TAIFA*